Msaada kupata kitambulisho cha NIDA

Msaada kupata kitambulisho cha NIDA

mbororo

Senior Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
103
Reaction score
88
Habar viongozi,

Msaada tafadhari mimi nililelewa na baba wa kambo na nikatumia majina yake kupata nida baadae

Baada kupata taarifa ya baba angu mzazi ikanibidi nitumie majina yake sasa nilisoma mpaka kidato cha nne.

Shida yangu ni kutaka kujua nitumie njia gani kubadilisha kutoka majina ya zaman katika nida na kutumia majina ambayo natumia sasa hivi msaada jaman nipo njia panda.
 
Kama upo Dar nenda kasajiri majina yako pale jengo baada ya mahakama kuu, ili majina yako mapya ndio yatambulike na utaomba kitambulisho kipya cha Nida.

Mwigulu Nchemba naye alikuwa na shida ya majina ametumia njia hiyo.
 
sasa mm tayar nina nida kwa majina mengne
 
Habar viongozi,

Msaada tafadhari mimi nililelewa na baba wa kambo na nikatumia majina yake kupata nida baadae

Baada kupata taarifa ya baba angu mzazi ikanibidi nitumie majina yake sasa nilisoma mpaka kidato cha nne.

Shida yangu ni kutaka kujua nitumie njia gani kubadilisha kutoka majina ya zaman katika nida na kutumia majina ambayo natumia sasa hivi msaada jaman nipo njia panda.
Utaratibu ni huu utaandaliwa deed poll zinakuwa copy 3
Utandaa passport size 3
Utandaa na copy ya kitambulisho
Gharama ya mwanasheria ni maelewano

Ukimaliza itapelekwa wizara ya ardhi ofisi ya msajiri wa nyaraka
Utalipia 32000

Utakaa siku 5 itakuwa tayari imesajiliwa

Utapeleka kwenda kutangaza kwenye gazeti la serikali shilingi 20000

Utakaa kama siku 5 hivi

Ukimaliza utaenda Nida utalipia 20000
Utajaza fomu ya kubadilisha majina

Na kazi imeisha hapo
Huo ndio mshakato boss
 
Back
Top Bottom