Msaada kutoka Brela

Arch Barrel

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2024
Posts
434
Reaction score
1,126
Wakuu habar za mchana, najua humu kuna account official ya Brela. Nahitaji msaada wa dharura

Kuna Agent nilimpa task ya kunifanyia annual filling na custom search, lakn mpaka sasa ni wiki ya 6 sipati majibu ya maana zaidi ya kuendelea kupoteza hela na muda huku hitaji langu likiwa linaendelea kuchelewa. Kazi hii nimewapa watu wawili kabla yake wakashindwa ndio nikaamua kumpa yeye. Lakn siku naambiwa network, mara ombi la awali limefutwa mpaka nashindwa kuelewa.

Nimeuliza ofisi zao za kanda kwa huku nilipo zinapatikana Mbeya na huku niliko ni mbali sana. Naomba kama kuna mtu anaweza kuniunganisha na mtu wa brela moja kwa moja anisaidie labda anaweza kunisaidia.

Hawa wa mtaani wamenichocha, wamekuwa wakinifanyia annual filling kila mwaka na nimekuwa nikilipia gharama. Lakn mwezi uliopita nilikuwa nahitaji Company search ili nipeleke mahali flani ili nipate huduma lkn cha kushangaza baada ya kuomba Company search ikaonekana sijawahi kufanya annual filling toka 2019.

Please wakuu naombeni msaada wenu
 
Tembelea tovuti ya Brela kuna mawasiliano yao wapigie
 
Tumia tax consultants yeyote atakufanyia .
Mkuu hao ndio wamenifikisha hapo. Wamefanya hiyo kazi, mpaka sasa nimelipia huduma ya annual filling kwa control number zaidi ya tatu lkn kila wakifanya company search inaonekana sijafanya return since 2019. Hiyo document nilikuwa naihitaji ili nipeleke bank lakn wananikwamisha. Bank wanahitaji Company search yenye current annual filling sio ya 2019. Naona wao ni kama wameshindwa.
 
Nimeelewa emu piga 0763666993 ukimaliza naomba mrejesho.
 

Habari, pole kwa changamoto uliyokutana nayo, tunaomba tutumie namba ya kampuni yako pamoja na jina la kampuni husika kwa njia ya ujumbe (DM) kwaajili ya msaada zaidi.
 
Ulishapata solution mtaalam? Kama bado tupigie 0743640640 kwa huduma za usajili wa biashara/kampuni/

Mimi ni Tax consultant. Nipigie 0743640640 tukusaidie. Pia kwa huduma za utunzaji wa nyaraka za fedha kwa ajili ya audit za TRA, Uandaaji wa hesabu zilizokaguliwa, n.k KARIBU TUKUHUDUMIE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…