Msaada kutoka kwenu wakuu

Msaada kutoka kwenu wakuu

albab

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,198
Reaction score
2,562
Wadau heshima yenu.
Kwa ufupi mwakani nataka nianze ujenzi ila bado napata ukakasi kuhusu haya yafuatayo.

1. Nitumie tofali za kuchoma (hapa nimepanga kujengea tope joint zikiwa ndogo saanaaa kwa haraka ukiangalia unaweza sema tofali zimepangwa tu)

2. Nitumie tofali za kupanga ("interlocking blocks" sijui ka nimepatia spelling) HIZI hutumia udongo wa kichuguu na cement kidogo sanaaa

Choma itanicost kwenye plaster wakati interlocking bila plaster naweza kuhamia na ikawa ka fashion nkizipaka polish....

Swali ni je UIMARA KWA AINA HIZI MBILI ZA TOFALI UKOJE????

Pichani inayopigwa lenta ni interlock hyo nyingine ni choma
 

Attachments

  • IMG_20201201_164510.jpg
    IMG_20201201_164510.jpg
    462.4 KB · Views: 8
  • IMG_20201201_171546.jpg
    IMG_20201201_171546.jpg
    279.3 KB · Views: 8
Tofali za kuchoma ni imara Mkuu.. ila hizo nyingine ni nzuri pia
 
Hizo tofari za kuchoma zikijengwa vizuri na tofari zikiwa aina moja haina haja ya plaster ya nje labda ndani tu..
 
Back
Top Bottom