Msaada: Kuwashwa na maumivu makali sehemu za siri wakati wa kujamiiana

Shmaider

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2015
Posts
406
Reaction score
120
Mchumba wangu anasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri na maumivu makali wakati wa kujamiana.

Naombeni msaada wa kitaalamu.
 
Hapo itabidi umshauri aende hospital huwenda akawa na magojwa y zinaaa
 
Kwa ndan kwa nje???

Fangas hao ...
Atumie antifungal dose
Flucan ya kumeza na ya kutumbukiza ukeni...
 
Alianza kuwashwa kwanje now mpaka kwa ndani
Fungus izo.... Nunua dawa ya fangasi ya kutumbukiza ukeni.kibox hakizid buku NNE ,then awe anatumbukiza kuanzia saa moja jion kwa siku ni kidonge kimoja na viko vitatu tu....

Flucanazole za kumeza kidonge kimoja buku nunua saba pamoja na panadol kwa siku ameze kimoja asubuh saa moja.... Then uone matokeo baada ya kumaliza dose inaondoa huo usumbufu kabsa....

Itapendeza na ww ukimeza dawa hizo ili usimwambukize mwenzio endapo amepona then ww ndo umebak na hzo fungus,,,,

Kingine kunyweni maji koz dawa ni kal na zinanguvu...
Pia nguo za ndan mkifua anikeni juan zikauke( msianike ndan)

La kuongezea kama itawezekana piga pasi chupi kabla hajaivaa ( au mnunulie chupi zingine) kama huwezi nunua dawa inaitwa Whitefield ya kikopo ndo itakaa mda mrefu awe anapaka mapajani akitok kuoga

La mwisho: mwambie mwanamke wako asioshee uke sabuni, atumie maji ya kawaida basi inatosha
 
Kama namwona vile. Wahi hosptl zi wazi 24 hrs. Unahc hayo maelezo yanatosha kumsaidia au uzembe wa kufikiri na kuamua.
 
Mchumba wangu anasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri na maumivu makali wakati wa kujamiana.

Naombeni msaada wa kitaalamu.
Atakuwa anayo maradhi ya Mzio (allergy) au Fungus sehemu zake za siri anitafute nipate kumtibia ili aweze kupona.


MUWASHO SEHEMU ZA SIRI BAADA YA TENDO
HUSABABISHWA NA NINI



Kujamiana ni kitendo cha heshima katika maisha ya ndoa ya binadamu. Ni tendo linalohusiana na uumbaji na kwa sababu wote tuliumbwa ni vyema tukaliheshimu kama tunavyojiheshimu wenyewe.



Kuna sababu kadhaa zinazosababisha tatizo la kuwashwa baaada ya kujamiana na mara nyingi tatizo hili huwatokea wanawake mara nyingi kuliko wanaume.



Kwanza kabisa wakati wa kujamiana tuangalie kama tuko wasafi, kwani jasho husababisha muwasho linapoingia ukeni. Mikono yenu wote ni misafi kwani huwezi kukumbuka umeshika nini kabla ya kukutana na mwenzio. Inawezekana ukawa umeshika pilipili na viungo vinavyowasha kama vitunguu na hukunawa vizuri.



Wanawake wanapojisafisha wanashauriwa kwa kutokea mbele kwenda nyuma ili kuepikana kuvutia uchafu wa sehemu ya haja kubwa kwenda ukeni kwani haja kubwa huwa na wadudu wanaoweza kuleta maambukizi ukeni.

Pili kuna mzio (allergy) ya mipira ya kiume au wa kike (Condom), mpira unaweza kuleta muwasho kama ngozi yako ina allergy ya mipira hii. Hii huwatokea baadhi ya wanawake wakati na baada ya kujamiana.

Allergy ya condom husababisha wekundu kwenye uke, kuwashwa na pengine kuvimba. Japo hali hii inaweza kupotea yenyewe baada ya muda mfupi lakini unashauriwa ukiwa nayo umuone daktari kwa ajili ya ushauri.

Allergy nyingine hutokana na mbegu za mwanaume. Kuna aina ya protini inayoweza kumkataa mwenza wako hivyo husababisha muwasho mkali wakati na baada ya kujamiana.
Hii ni mbaya zaidi kwa sababu mwanamke wakati mwingine anaweza kuwashwa mwili mzima na hata kushindwa kupumua vizuri kumuona daktari ili huduma ya haraka itolewe.

Muwasho mwingine unaweza kutokana na magonjwa ya zinaa, miwasho ya magonjwa ya zinaa haitokei mara moja wakati wa kujamiana na pengine inaweza kuchukua saa nyingi na siku kadhaa baada ya kufanya tendo hilo.

Miwasho ya magonjwa ya zinaa inaweza kuambatana na uchafu kutoka ukeni, vipele sehemu za uke na hata wakati mwingine mwanaume anaweza kuumwa tumbola chini ya kitovu.
unashauriwa kumuona daktari ukionadalili hizi mara moja ili kujikinga na maambukizi zaidi. Magonjwa ya ya zinaa yakiwa sugu yanaweza kusababisha ugumba kwa mwanamke hata mwanaume.

Kuna fangasi ambazo hutokea sehemu ya uke na muwasho wake huongezeka pale pindi utakapokutana kimwili na mwanaume, fangasi zinaweza kupona kwa dawa na pia kuzingatia usafi na kuvaa nguo kavu na zilizoanikwa juani au kupigwa pasi.

❎Usiweke nguo za ndani chini ya godoro kwani ni rahisi kuotesha fangasi.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…