Ushetu moja ya wilaya mpya iliyomengwa kutoka wilaya ya Kahama, hivyo maisha yako yatakuwa kahama, wakaazi wa kahama wanasema huduma zote zilizoko Dar zipo Kahama pia. Kwa mfano benki zote zipo, hotel za mpaka 200,000 zipo. mkuu hutajuta ukifika.
Umepangiwa nini, mwalimu au kidato cha tano? weka wazi ndugu tukusaidie, mimi ni mzaliwa wa kahama. Ushetu ni halmashauri mpya ambayo ilikuwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya kahama. Kwa sasa wilaya ya kahama imezaa halmashauri tatu ikiwemo ya Ushetu, Msalala na Halmashauri ya kahama mji. Ushetu ni halmashauri changa ipo kama km 80 au 70 kutoka kahama mjini. Hata hivyo kwakuwa bado ni changa, mambo ya kiutendaji (utawala) na ofisi zote bado zipo kahama mjini, na ushetu ilipewa ofisi zile zilizokuwa zinatumika na iliyokuwa halmashauri ya wilaya ya kahama. Ofisi zipo karibu na Hospitali ya Wilaya au karibu na kanisa la Roma (jimbo katoliki la kahama) Ukifika hospitali ya wilaya ya kahama, uliza halmashauri ya ushetu utaelekezwa, au ofisi ya mkuu wa wilaya. Karibu mkuu