Msaada kwa anayejua dawa ya kuondoa weusi chini ya macho

Msaada kwa anayejua dawa ya kuondoa weusi chini ya macho

Inamonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2016
Posts
779
Reaction score
474
Habari ndugu zangu..
Naomba msaada wenu kwa anaye jua dawa/lotion/sabuni ambayo itanisaidia kuondoa weusi chini ya macho..
 
Hizo lotion zinazochubua ndo zinakupa huo weusi acha kutumia utakuwa Na rangi yako ya asili Na weusi utapotea
 
Kama ndio ulivyozaliwa basi hakuna dawa na kama ni kutokana na kujichubua hapo kazana na vitu vya asili tu, liwa na manjano, matokeo ni taratibu ila kama una nia utatoboa.
 
Hapana sijawahi kujichubua.
na hali hii imeanza kunitokea mwaka huu..
 
Basi dawa ndio hiyo... japo anzia kwanza kwa daktari wa ngozi ijulikane tatizo lake nini labda unavaa sana miwani.
 
Hapana sijawahi kujichubua.
na hali hii imeanza kunitokea mwaka huu..
Kama haujichubui na wala haupaki lotion kali kuna makala nilisomaga weusi chini ya macho uswahili tunasema miwani inaweza kusababishwa kuto lala usingizi wa kutosha binadamu anapaswa Kulala masaa 8 hata 7
 
Unaweza kuchukua kiazi mbatata usikimenye kikate kati halafu kata tena kiasi chembamba cha kiazi kama ulivyokata mwanzo lakin kiwe chembamba kata mara 2 weka kwenye macho yako ukiwa umeyafumba vizuri zoezi hili lifanyike usiku wakati wakulala na unaweza kutumia tango pia utafanya kama kiazi mbatata kwa maelekezo zaid ingia youtube tafuta wana njia nying utachagua upendao
 
Back
Top Bottom