Msaada kwa anayejua njia rahisi ya kupokea mizigo kwa airline kutoka Uk.

American nigga

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
673
Reaction score
974
Samahani wadau wangu wa JF nina shida ndugu zangu nahitaji mtu yoyote anayejua njia rahisi zaidi ya kupokea mizigo kutoka UK kwa njia ya anga, nahitaji sana msaada wenu ndugu zangu.
 
Powa, London yupo mtu anasafirisha kwa kilo £4 kwenda zanzibar, Dar ni £5 kwa kilo, kufika mzigo ni week moja tu. Ndio njia rahisi sana
 
Powa, London yupo mtu anasafirisha kwa kilo £4 kwenda zanzibar, Dar ni £5 kwa kilo, kufika mzigo ni week moja tu. Ndio njia rahisi sana

anaitwa nani? ana kampuni? kampuni yake inaitwaje? ana uzoefu wa muda gani na sisi tunaweza kumwamini vipi? ana ofisi dar? hata godoro anasafirisha kwa 5GBP kwa kilo? nina magodoro ishirini nataka kuyasafirisha november.
OP: tumia njia zote lakini epuka sana Fedex, wakala wao wa dar kaajiri genge la vibaka kazi yao ni kukwapua parcel wanazohisi ziko valuable, pesa wanagawana na mabosi wao halafu wewe wanakuchinjia baharini.
 

Mkuu godoro halisafirishwi kwa ndege ila kama kamzigo kako kadogo kama box na Vitu vyengine bei ndo hio, kuna mizigo huwezi kusafirisha kwa ndege ni gharama kubwa, kwa ushauri magodoro ni contena, huyo mtu yupo barking, East London.
 

Mimi huwa napata order ya Vitu mbali mbali hasafirisha kwa njia hio ya ndege hata mabegi ya nguo,spare parts, na Vitu vyengine.

Mizigo kama magodoro, machine, Vitu vya electronic ambavyo ni vingi kwa biashara , huwa nafunga kwenye box na kusafirisha kwa contener, charges kama £10-£30 Inategemea na ukubwa.
 
mbona kuna member humu Lukosi nadhani anaitwa wanafanya hiyo shughuli
 
Mkuu godoro halisafirishwi kwa ndege ila kama kamzigo kako kadogo kama box na Vitu vyengine bei ndo hio, kuna mizigo huwezi kusafirisha kwa ndege ni gharama kubwa, kwa ushauri magodoro ni contena, huyo mtu yupo barking, East London.

nashukuru mkuu kwa ufafanuzi, maana nilivoskia 5gbp kwa kilo bila kuspecify kwamba inategemea upana wa mzigo nikajua "bingo". haujajibu suala la ofisi mkuu, wana ofisi dar?
 
I think ndo itakavyo kuwa, mimi mizigo yangu inamalizia zanzibar, lakini dar pia wanapeleka, wanao safirisha hawa ni self employment, hivyo kwa hapa uk hawana official office, lakini wanapatikana katika makazi yao,niliwahi kuona kina dada kutoka bara na mizigo mingi ya box na baggage
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…