Msaada kwa comb ya HGE

Siyo kana kwamba siwez math kaka! Ila siuna jua tu necta... math naiweza

F bado unaweza Maths,? angalia comb nyingine itakusumbua kuingia chuo Unless umeresit maths
 
MIMI NI MWL. WA SHULE MOJAWAPO Tz AMBAYO INA ADVANCED LEVEL TU! SO NAFAHAMU

Na ualimu wako wote hapa UMEDANGANYA!!! Si kweli mwanafunzi kupata f au d ya somo useme ashindwe kusoma somo husika advance!!! Nyie ndio sampuli ya waalimu msiojua nini maana ya elimu!!
 

Mkuu medyzo pitia huu ushauri...
 
Last edited by a moderator:
Mmmmmh! Mbona mnanitisha aiseeeeee

Usitishike ndugu yangu hii ndio dunia na watu kama hawa wapo!!!

Labda nianze kwa kukupongeza kwa kuwa na moyo huo wa kuendelea kusona math (bam) bila kujali historia yako!!! Kwa hilo hongera sana!!!

Kusoma kwa levo ya advance na olevo ni tofauti sana!!! Kama mdau alivyosema hapo juu, binafsi nakushauri uende hge!!! Kwanini????

Kama unaipenda hge, kama unapenda uchumi nenda kasome ndugu yangu hamna linaloshindikana kama tu utakua na nia thabiti katika masomo yako!!!

Kuna mifano hai kabisa watu walikua na f za maths ya olevo na wakaenda private kusoma maths tena pure maths na mwisho wa siku wakapiga one kali na hapa nnavoandika wapo vyuoni na wanakimbiza kama kawaida!!!
medyzo ukianza kuangalia ulipata nini kamwe hutafika kwa sasa focus kwenye "unataka nini hasa katika maisha yako ya baadae"!!!

Ukiwa na nia(passion) toka moyoni hakuna linashindikana hata kama watu au wenzio watakukatisha tamaa!!!

Utapata mawazo mengi sana na mengine ya kukutasha tamaa, lakini amini nakwambia f yako ya form four isiwe kikwazo katika future yako!!!

Ipende hesabu hasa utapoenda form5 amin lazima tu utafanikiwa!! Achana na historia angalia maisha yajayo na mtu asikukatishe tamaa!!! Kila la heri na maandalizi mema ya form5!!
 
Last edited by a moderator:
Samahani wakuu mim ni kijana niliye maliza form 4 mwaka jana 2013, sasa ninaipenda comb ya HGE napenda sana kusomea uchumi
Sasa kulingana na matokeo yangu Mathematics nimepata F, vp ninaweza kusoma comb hiyo..?

Kwa private school unaweza enda soma HGE pamoja na kupata F ya math o-level na ukamudu vizuri sana.

Lakini sasa ukiendelea kusoma uchumi chuoni au fani nyingine zinazofanana na hizo itakusumbua sana kwenye ajira na hiyo ''F ya Maths ya O-level''.
 

Asante sana kaka kwa ushauri wako mzuri tena wenye mashiko. Nimefurahi sana kuwa umenichukulia kama mdogo wako! Kwa kunipa ushauri wa kina na wakisomi zaid! Nakuahid nitayafanyia kazi mawazo na mchango wako!
 
Last edited by a moderator:
Kwa private school unaweza enda soma HGE pamoja na kupata F ya math o-level na ukamudu vizuri sana.

Lakini sasa ukiendelea kusoma uchumi chuoni au fani nyingine zinazofanana na hizo itakusumbua sana kwenye ajira na hiyo ''F ya Maths ya O-level''.

Ok! Asante kaka ko wew unanishaur labda nikifanikiwa kwenda chuo kwa hge hiyo unanishauri nisomee Fani gani"?
 
Hapana kaka katika hge

>>>> hiyo E ni Economy

its economics brother.

halafu kumbuka kuwa baraza la mitihani la taifa ndiyo kipimo cha kufaulu ama kufeli.

kupata kwako F katika mathematics inathibitisha kuwa huna sifa za kusoma HGE wala usilazimishe kuwa unajua hesabu.

huna sehemu nyingine ya kujitetea, btw, mlishushiwa sana grades kwa mwaka wenu mpaka 19, mpaka hapo ukafeli?
 
Siyo kana kwamba siwez math kaka! Ila siuna jua tu necta... math naiweza
nenda private baadhi ya shule wanachukua tu,nimesoma na wengi tu hge.HGE wengi kwanza huwa wanakimbia bam ila ukitaka upate course nyingi chuo BAM usikimbie ndugu.tafuta shule ya private kwa gvt sidhani
 
sikuhizi BAM kuna section a tu na unajibu maswali yote kumi tu.ni simple ukifuatilia na ku solve maswali mengi.kijana kakomae maana wengi huwa wanadharau BAM.jamaa yangu o level katoka na A Ya hesabu,kapiga PCB KATOKA NA mswaki wa BAM
 
samahani wakuu mim ni kijana niliye maliza form 4 mwaka jana 2013, sasa ninaipenda comb ya hge napenda sana kusomea uchumi
sasa kulingana na matokeo yangu mathematics nimepata f, vp ninaweza kusoma comb hiyo..?
pia mtoa maada kama unandoto na uchumi basi anza twishen ya crash kama inawezekana ,advance kasome bam kwa msuli wa kupata a hata kama wanaweka s .lasivyo pure economics is like a pure science .kuna mahesabu balaa jamani.yaani mtu unabadilika kuwa calculator.,,,..econometrics???/
 

Aliye kudanganya nan...? Hiyo 19 unayo isemea wew ni F alama D inaanzia 30
 

Haaaaaahaaaaa! Asante kaka
 
kiukweli, moja ya vigezo vya kusoma combinations kama HGE,EGM,CBG, & PCB ni lazima uwe umefaulu maths..kwa sisi tuliosoma kabla ya huu mfumo mpya ni lazima uwe umefaulu kuanzia grade "D" kwenda juu yaani C,B, na A.
 
Umeni-quote vibaya! Kwa uchumi ni lazima ufaulu hesabu, ila kwa masomo mengine sio lazima ...kwa mfano hgk sio lazima ufaulu english! Akili yako mgando kama ya c..m!
na ualimu wako wote hapa umedanganya!!! Si kweli mwanafunzi kupata f au d ya somo useme ashindwe kusoma somo husika advance!!! Nyie ndio sampuli ya waalimu msiojua nini maana ya elimu!!
 
Asante sana dada angu kwa kunitia moyo! Mungu akutangulie

Amina kapige tu msuli me mbona wapo niliosoma nao ECA walikuwa na F za hesabu na wapo wa HGE pia wenye F za hesabu na necta wakatoka na S... Tena ni govt school.. Suala la kuchaguliwa inayegemea na ufaulu wakiwa wachache hata wenye F serikalini wanachukuliwa kusoma HGE au ECA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…