Msaada kwa hili linalonitesa

Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
269
Reaction score
71
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 Nina mke mmoja ambaye ni mjamzito, Tatizo langu maisha yangu yamekuwa na mikosi au kivingine mazingaumbwe, kila napofanikiwa kidogo napata matatizo makubwa sana kama kutokewa na nguvu za giza ndotoni au hata nikiwa kwenye pilikapilika.

Juzi kati Rafiki yangu tuliyekuwa tunafanya wote biashara kanitoa ofisini na kuniambia fanya mambo yako nami nifanye yangu baada ya biashara kukua sana ila pesa aliyonipa ni Mungu tu ndo anajua, Kanidhulumu na siwezi kumshtaki kwani hatujaandikiana.

Naombeni ushauri wenu kwa yoyote atakayekuwa na wazo la kunisaidia kwani sasa hivi sina chochote na huku mke wangu akikaribia kujifungua. Nimekata tamaa sijui nifanye nini?

Ila baada ya kutembelea hili jukwaa nikahamasika na ushauri unaotolewa, Nikaona kuliko kukaa kimya bora niombe msaada wa kimawazo kwenu.

Asanteni sana kwa msaada wa kimawazo mtakaonipa.
 
Yaani kila napotaka kupiga hatua moja mbele, mambo yangu yote huaribika,
 

Maelezo yako hayajajitosheleza kijana, upo wapi??, unataka msaada gani?? Umedhurumiwa sawa ila umepewa kiasi gani katika dhuruma iyo??, umejaribu kufikilia ww kwa upeo wko unataka kufanya nn??
 
Mkuu ili upate msaada zaidi hii kitu yako ipeleke jukwaa sahihi.
Huku ni matibabu tu
 
Maelezo yako hayajajitosheleza kijana, upo wapi??, unataka msaada gani?? Umedhurumiwa sawa ila umepewa kiasi gani katika dhuruma iyo??, umejaribu kufikilia ww kwa upeo wko unataka kufanya nn??

Nipo Makongo, kiasi nilichopewa 350000, msaada naotaka ni ushauri binafsi kama labda imekutokea wewe ungefanyaje? Mimi kama mimi kweli sijui nifanyeje ndo maana nimeomba msaada wa kimawazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…