Kwa wenye uelewa, nini chanzo na ipi ni tiba ya matatizo ya dada huyu?
1. Anapata maumivu makali wakati wa hedhi
2. Mwezi huu hajaingia hedhi, maumivu yemekuwa makali zaidi, maziwa nayo yanauma (kapima mimba hamna)
3. Anakojoa kwa shida ingawa mara kwa mara anahisi kutaka kukojoa, hata akienda kukojoa anaweza kukojoa mkojo ukakatika ghafla mpaka baada ya dakika kadhaa ndio anakojoa tena
4. Anasikia maumivu makali kwenye nyonga pande zote yanayokatiza kwenye kibofu, pamoja na kiuno kwa ujumla.
Amepima UTI hamna kitu. Msaada wenu ni muhimu sana, Natanguliza shukurani.