Msaada kwa mama mwenye mtoto.

magila

Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
37
Reaction score
4
Habari zenu wana bodi!

Kuna mwana mke ambae ana mtoto wa miezi mitano, bahati mbaya baba wa mtoto hakukubali kuishi tena na yule mwanamke baada ya kujua ana ujauzito. Huyu mwanamke alipata Boyfriend ambae yupo nae hadi ivi sasa na hawajawai kufanya tendo la ndoa. Lakini siku za hivi karibuni amekua nahisia kali sana za kuhitaji akutane na huyo boyfriend wake kimwili. Je? Kuna madhara yanayoweza kutokea kwa mtoto kwa kufanya hilo tendo na kama yapo ni njia gani anaweza kufanya ili ku yaepuka pia hata kukabiliana na iyo hali.


N:B maziwa ya mama wa mtoto pia hayatoki.

Jumatatu Njema!

Copy:
MziziMkavu
gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.@magila ikiwa maziwa ya mama hayatoki anaweza kufanya mapenzi lakini kwanza waende kupima ukimwi na avae soksi akifanya hayo mapenzi kuepusha kupata mimba na Maradhi.
 
Hivi ile kitu kubemenda mtoto inatokana na nini..!??
 
Hivi ile kitu kubemenda mtoto inatokana na nini..!??
hapana sio hivi
Ni kitendo cha mwanamke alie zaa kufanya mapenzi na mtu ambae ni tofauti na baba wa mtoto original. Hii inaweza ku athiri hata ukuaji wa mtoto.

iko hivi, mtoto huwa habemendiki kwasababu ya kufanya tendo la ndoa lahasha. Ila mtoto huwa anawa mnyongefu kwa kukosa huduma mauahimaua toka kwa mzazi wake wa kike kama vile kubebwa, kulishwa kwa wakati, uchafu nk. Mama anayelea mtoto mdogo anapaswa amudu kutunza ama kulea watoto wawili yaani mtoto mdogo na mkubwa kwa wakati mmoja.

inapaswa akumbuke kwamba mtoto mdogo yuko prone to infection so usafi, kulishwa kwa wakati, kulala vizuri,kubembelezwa kupewa attention ni jambo la muhimu sana kwa mtoto huyu. Mama akiendekeza kumlea baba tu wakabaki wamekumbatiana mwanzo mwisho katoto kakaachiwa baridi katapata pneumonia, mama na baba wasipojiswafi baadaya tendo vyema wakamkumbatia mtoto watampa infection, mtoto asipolishwa ama kunyonyeshwa maziwa safi nikiwa na maana titi limeoshwa vyema halina jasho wala shahawa ama marashi mtoto huyu anaweza kuhara.

ikumbukwe kwamba kubemenda tunakoongelea ni kule kwa mtoto kukalia mgongo, miguu kulegea kuharisha uharo ukatokea mbeleni nk lkn yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya ishe duni, na uchafu. mtoto asipopata calcium ya kutosha miguu haiwez kukaza na akikaa mgongo utajipinda, kuhara ni wazi kwamba mtoto kala mavi kudhoofu huletwa na kuhara na vijihoma bavyo humwandama mtoto kwa kukosa matunzo stahili.

Hivyo ni wajibu wa wenzi kuwa makini kipindii cha malezi ya mtoto wao mdogo ili kumkuza salama huku akifurahia maisha yao ya kula tunda. kwa mtu kama mimi huwa naona ni busara, zaid japo ni abstain kwa muda wa miezi hata 3 ili mtoto nimkomalie akomae kidogo kabla sijarudisha huduma za baba kwa asilimia mia. hii hunifanya mtoto awe mnene na awe na afya njema zaidi.
 
Mfano mie, na mke wangu kajifungua, alafu mke wangu akawa anafanya mapenzi huko mtaani na mwanaume mwingine tofauti, kuna madhara yanayoweza jitokeza?






 
Mfano mie, na mke wangu kajifungua, alafu mke wangu akawa anafanya mapenzi huko mtaani na mwanaume mwingine tofauti, kuna madhara yanayoweza jitokeza?

huyu mama akifanya hivyo wala hawez kumfanya mtoto apate shida so long as atakuwa msafi, na anajali. Kumbuka kwamba mama lazima atatumia condom so hata chances za kuwa mimbad ni ngumu. But siyo busara kufanya hivi kwani ni kuwatesa watoto wako na mwenzi wako kihisia
 
Nimekuelewa mama,

Shikamo mama yangu mpenzi!
Siku njema na kazi njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…