Mgongo wa paka
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 485
- 36
Wana JF
Ninaishi Dar es Salaam. Nina ardhi ya kutosha Mpwapwa, Kongwa, Malinyi na Kilombero. Baada ya kufanya research ya kutosha, nimeamua niingie kwenye kilimo na ufugaji mkubwa wa kisasa ili kupunguza msongo wa kusubiria mshahara mwisho wa mwezi. Tractor nimeshaagiza Japan lipo njiani linakuja. Nina mpango pia wa kuwa na mashine ya kuvunia mpunga hapo baadaye. Kukamilisha mradi huu ili uweze kuanza,ninahitaji mkopo wa Tsh Ml. 80 mpaka Ml.100. Dhamana ninazo namaanisha Hati za nyumba zangu 4 hapa Dar es Salaam. Nimejaribu kupita katika baadhi ya Benki, wanasema wao wanakopesha wafanyabiashara wakati mimi si mfanyabiashara. Hivyo natafuta mtu yeyote ambaye ni mfanyabiashara mwenye transactions nzuri za walau Ml 10 kwa kila mwezi, nimpe Hati ya nyumba yangu moja aende Acces Bank akakope maana Acces Bank wanakubali mtu kukopa kwa dhamana ya mtu mwingine. Likikamilika hilo asante yangu nitatoa Tsh.Milioni 3 cash
Hivyo naomba kwa yeyote mwenye sifa hiyo, anitafute kwa namba ya simu 0767 87 60 86 ili tufanye mchakato
Shukrani
Mkuu The Boss nipo serious pasipo shaka kabisa
Wana JF
Ninaishi Dar es Salaam. Nina ardhi ya kutosha Mpwapwa, Kongwa, Malinyi na Kilombero. Baada ya kufanya research ya kutosha, nimeamua niingie kwenye kilimo na ufugaji mkubwa wa kisasa ili kupunguza msongo wa kusubiria mshahara mwisho wa mwezi. Tractor nimeshaagiza Japan lipo njiani linakuja. Nina mpango pia wa kuwa na mashine ya kuvunia mpunga hapo baadaye. Kukamilisha mradi huu ili uweze kuanza,ninahitaji mkopo wa Tsh Ml. 80 mpaka Ml.100. Dhamana ninazo namaanisha Hati za nyumba zangu 4 hapa Dar es Salaam.
Nimejaribu kupita katika baadhi ya Benki, wanasema wao wanakopesha wafanyabiashara wakati mimi si mfanyabiashara. Hivyo natafuta mtu yeyote ambaye ni mfanyabiashara mwenye transactions nzuri za walau Ml 10 kwa kila mwezi, nimpe Hati ya nyumba yangu moja aende Acces Bank akakope maana Acces Bank wanakubali mtu kukopa kwa dhamana ya mtu mwingine. Likikamilika hilo asante yangu nitatoa Tsh.Milioni 3 cash.
Hivyo naomba kwa yeyote mwenye sifa hiyo, anitafute kwa namba ya simu ili tufanye mchakato.
Shukrani
Anachosema ni kweli. Bank zetu bado hovyo sana. Hawakopeshi kma dhamana ya kuweka aldhi,nyumba,gari au assets nyingine. Nimewahi taka just 10m kwa haraka na ningerudisha ndani ya 2months.nikawapelekea gari ya sh 25m na kadi yake. Wakakataa!Hizo hati ni zako kweli au ni za nyumba ya mtu
mwingine ? Maana kama una hati kweli Benki hawashindwi kukukopesha fedha ndogo kama hizo
Wana JF
Kwa mlionishauri niende TIB Bank dirisha la kilimo nimeenda leo. Mlolongo wa pale si wa kitoto. Masharti ni mengi zaidi ya ya World Bank kama si IMF.Kwa mliohoji kuhusu uhalali wa hati ni kwamba nyumba zote zina hati na Hati zipo kwa jina langu mimi mwenyewe na si jina la mtu mwingine. Kwa walionishauri suala la kuuza nyumba moja nimeafiki wazo hilo so natangaza kuuza nyumba moja iliyopo eneo la Madale kwa bei nzuri tu. Kiwanja kina ukubwa wa Square Meter 1203 na hati ya umiliki ya miaka 33.
Kwa aliye serious tuwasiliane
Shukrani