Msaada: Kwa mnaoagiza vipodozi nje ya nchi TFDA na TBS inakuaje hapo?

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Habari wapendwa

Kwa mnaoagiza vipodozi kutoka nje ya nchi na kutumiwa hapa namaanisha wale wanaotumiwa kupitia dhl,meli,ndege etc

Nimeambiwa ni lazima zikaguliwe na TFDA na TBS na pia nimeelezwa kuwa ni lazima kwa zile husika huko vipodozi vyako vinakotea uwe pia na na vyeti vyao vya uthibitisho wa mamlaka za huko

Sasa hii imekaaje wadau nataka nianze kuagiza vipodozi mpk piece 100 kwa kuanza ila sasa mimi cheti cha nchi husika nitakipata wapi lakini katika mitandao muuzaji kaambatanisha vyeti vya uthibitisho kuwa vipodozi viko verfied na mamlaka husika za huko na hapa kwetu ukaguzi unakuaje?,maana nahisi itakua ni kuzungushwa tu

Mnaonunuaga tafadhali nishaurini na hata mnaojua pls
 
Nenda TBS upate maelezo ya uhakika.
 
Huwezi pata vibali Kwa wakati na unaweza usipate kabisa kama wewe ni muagizaji mdogo. Nenda mipakani mwa nchi Kisha ongea na wadau watakuelekeza njia rahisi.
 
Huwezi pata vibali Kwa wakati na unaweza usipate kabisa kama wewe ni muagizaji mdogo. Nenda mipakani mwa nchi Kisha ongea na wadau watakuelekeza njia rahisi.
Asante
 

Unataka kuagiza vipodozi gani?Kutoka nchi gani?Kma ni kutoka Uchina ninaweza kukusaidia,ila kama ni kutoka nchi nyingine sina uzoefu nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…