Msaada kwa mwenye utaalamu wa biashara ya juice fresh za matunda?

KJ07

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2021
Posts
2,370
Reaction score
5,381
Habari wakuuu.

Nimekuja mbele yenu kutaka msaada kwa mwenye ujuzi wa biashara ya juice za matunda fresh location ni Dar.

Je, ni zipi changamoto za biashara hii.

Je, soko lake likoje na ni kwa namna gani naweza kuingia katika soko la ushindani.

Je, mtaji ambao unaweza kuendesha biashara hii ni kiasi gani na vitu gani muhimu vya kuwa navya kabla sijaanza biashara hii.

Je ni juice gani ni pendwa kwa jiji hili la Dar?

Je, Ntawezaje kujitofautisha na watu wengine ambao wanafanya biashara hii.?

Kwa mwenye ujuzi karibu tushare mawazo.

Natanguliza shukrani.

Naomba kuwasilisha.
 
1. Changamoto za biashara ya juice.
Inategemea unataka kuifanya katika level gani.
kama unaanza kwa kutembeza barabarani basi anza na dumu 2 lenye ladha tofauti, mwengine atataka umchanganyie, mwengine atapenda moja zaidi.
Pia jitahidi iwe imeganda vizuri maana wanywa juice wanapenda ikiwa ya baridi.
Pia hakikisha usiuze juice iliyolala ili kuepusha mtu kuumwa tumbo na kukosa wateja.

Kama unakibanda cha kuuzia juice basi hakikisha umeme uwepo, fridge liwepo, mabarafu ya kusagia yawepo na blender yako iwe kubwa na uwe msafi mno.

2.Soko
Huwezi kosa soko la juice kulingana na hali ya hewa ya Dares Salaam, sema inategemea na vionjo utakavyoviweka kwenye juice yako na bei pia, hakikisha kila mmoja mwenye 500 hakosi na mwenye 5,000 hakosi juice.

3. Mahitaji
Blender heavy duty zuri zaidi na litadumu, vipackage vizuri, mirija, fridge, maji masafi, chujio, vyombo vyengine

4. Juice pendwa ni Maembe, maparachichi, passion, ukwaju, ubuyu, rosella, juice ya tende, juice pendwa ya miwa na smoothies

5. Consistency (hata ikitokea hujapata wateja kwa ukubwa uliotegemea hakikisha unaamka asubuhi na kwenda kufungua biashara)
Pia unaweza kutoa sample za kuonjesha watu mwanzoni ili wajue jinsi juice yako ilivyo tamu
Weka lebel kwenye vikopo vyako vikiwa na jina lako la biashara
Buni juice yako ambayo ndio inaweza kuku introduce vyema kwenye market, huenda ipo lakini ongeza kitu kidogo
 
tamu

Shukrani mkuu kwa nondo zako
 
Usafi usafi usafi, juice inahitaji usafi mnoooo ndo mana nikiona inauzwa glass 500 nakimbia maana kwa garama zake kutengeneza mpka kufika sokoni si mchezo, uwe na gloves za plastic, uwe na kucha fupi safiiiiiiii, usiwe unatoka jasho uku unaserve au kuteneza, ukiwa unatengeneza usiongee kabisa mahali unapotenezea pawe rasmi vyombo rasmi masi safi na salama.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Muhimu location
Pia inategemea una kiasi ambacho unataka kuwekeza
Vifaa vya kutengenezea na freezer/ fridge na pia kwa kuongeza unaweza kuanza kutengeneza Ice cream zako mwenyewe na ukaweka chata zako
 
  • Thanks
Reactions: apk
1. Changamoto za biashara ya juice.
Inategemea unataka kuifanya katika level gani.
kama unaanza kwa kutembeza barabarani basi anza na dumu 2 lenye ladha tofauti, mwengine atataka umchanganyie, mwengine atapenda moja zaidi.
Pia jitahidi iwe imeganda vizuri maana wanywa juice wanapenda ikiwa ya baridi.
Pia hakikisha usiuze juice iliyolala ili kuepusha mtu kuumwa tumbo na kukosa wateja.

Kama unakibanda cha kuuzia juice basi hakikisha umeme uwepo, fridge liwepo, mabarafu ya kusagia yawepo na blender yako iwe kubwa na uwe msafi mno.

2.Soko
Huwezi kosa soko la juice kulingana na hali ya hewa ya Dares Salaam, sema inategemea na vionjo utakavyoviweka kwenye juice yako na bei pia, hakikisha kila mmoja mwenye 500 hakosi na mwenye 5,000 hakosi juice.

3. Mahitaji
Blender heavy duty zuri zaidi na litadumu, vipackage vizuri, mirija, fridge, maji masafi, chujio, vyombo vyengine

4. Juice pendwa ni Maembe, maparachichi, passion, ukwaju, ubuyu, rosella, juice ya tende, juice pendwa ya miwa na smoothies

5. Consistency (hata ikitokea hujapata wateja kwa ukubwa uliotegemea hakikisha unaamka asubuhi na kwenda kufungua biashara)
Pia unaweza kutoa sample za kuonjesha watu mwanzoni ili wajue jinsi juice yako ilivyo tamu
Weka lebel kwenye vikopo vyako vikiwa na jina lako la biashara
Buni juice yako ambayo ndio inaweza kuku introduce vyema kwenye market, huenda ipo lakini ongeza kitu kidogo
Mkuu una sehemu ya biashara hii?
 
Mkuu una sehemu ya biashara hii?
Blender heavy duty zinapatikana wapi? Nyingi zilizoko kwenye maduka, zinaitwa heavy duty lakini siyo... Na vifungashio vinapatikana wapi?? Kuepuka kutumia chupa zilizotumika za maji au vinywaji vingine
 
Vifungashio vipo Kila mini Supermarket
 
Blender heavy duty zinapatikana wapi? Nyingi zilizoko kwenye maduka, zinaitwa heavy duty lakini siyo... Na vifungashio vinapatikana wapi?? Kuepuka kutumia chupa zilizotumika za maji au vinywaji vingine
Mkuu mimi siishi huko ila kwa huku nilipo zipo za kila aina na og pia
Kwa mfano hii hapa ni £150 kama laki 5 na ina 2000w
Screenshot_20240129_123518_Amazon Shopping~2.png
 
Back
Top Bottom