Msaada kwa tatizo la mtoto wa miaka 4.5

Msaada kwa tatizo la mtoto wa miaka 4.5

MKOBA2011

Senior Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
142
Reaction score
27
Wanajamii forum habari za shughuli?Aisee naomba msaada kwa mtu anayejuwa tiba ya mtoto mwenye umri wa miaka minne na nusu katika mfumo wa kupumua yaani anapumua kwa kuweka kituo between two hurt beat sasa nimetumia baadhi ya dawa sioni mabadiliko yeyote naomba kama kuna mtu anayejuwa tatizo hili husababishwa na nini na tiba yake ni nini anijuze wadau
 
Pole mkuu,

Upumuaji wake uko hivyo toka lini(kwa muda gani sasa)?
Je, kuna wakati upumuaji huo inazidi sana? ni muda upi usiku au mchana?
-Kuna ukaaji(mkao) wowote unaomsaidia mtoto,upi?
-Kuna dawa zozote anazotumia kumsaidia?

-Je, mtoto ana tatizo jingine tofauti na hilo mf. Homa(joto kali/dogo la mwili)? Kukohoa, Kutapika, kuharisha, vifundo kuuma n.k?

-Vipi katika familia(upande wa mzazi wa kiume na wa kike) kuna mtu/ndugu mwenye/aliyekuwa na ugonjwa wa Pumu(Asthma), Moyo?!

USHAURI:ni vizuri kufika hospitali mapema(matibabu ya watoto chini ya miaka mitano(5) ni bure kulingana na sera ya Taifa so utahudumiwa mapema.
 
Nashukuru kwa ushauri mpaka ni kuwa tatizo si la muda mrefu ni kama three weeks na katika ukoo akuna mtu mwenye tatizo hilo na sasa yupo kwenye dozi za antibiotics ameanza juzi kwa hiyo tunaangalia maendeleo yake kwa ushauri wa madaktari na mara nyingi hali inakuwa mbaya usiku mchana kunakuwa na unafuu kidogo
 
kwenye kupumua anabanwa pumzi au akipumua kawaida anaweka kituo usikute pumu inamnyemelea au mafuta yameziba vimishipa vya damu hivyo kusababisha inashindwa kupampu vizuri na kupitisha damu vizuri kwenda kwenye moyo
kitu cha kufanya hili kumpima mpandishe ngazi ndefu au apande kilima alafu mpime utoaji wake pumzi kama mtu aliyeishiwa na pumzi au anahema kawaida lakini kama anatafuta hewa halafu njoo unipe feedback nitajua nini cha kukushauri
 
Naomba uende peramiho kuna Dr mzuri moyo na the like amwone mwanao. Pole sana
 
kwenye kupumua anabanwa pumzi au akipumua kawaida anaweka kituo usikute pumu inamnyemelea au mafuta yameziba vimishipa vya damu hivyo kusababisha inashindwa kupampu vizuri na kupitisha damu vizuri kwenda kwenye moyo
kitu cha kufanya hili kumpima mpandishe ngazi ndefu au apande kilima alafu mpime utoaji wake pumzi kama mtu aliyeishiwa na pumzi au anahema kawaida lakini kama anatafuta hewa halafu njoo unipe feedback nitajua nini cha
kukushauri
Omega naomba ushauri now imetokea kama ulivyosema kaka
 
kaka nakuomba ujibu maswali wanayayokuuliza ndo utasaidia maana kila una dalili zake ukijibu maswali madaktari ndo tunajua tatzo.
1.angalia mtoto anapata homa...?
2. Mtoto anakohoa?
3. Anatatizo la moyo tangia mdogo
4. Je ashawai kuchange rangi mfano kuwa wa blue.!
5. Anakula vzuri. Vp ukuaji wake
kama wenzangu walivyo sema. Kiasi kikubwa hyo ni. @ pneumonia, inapona kwa antibiotic inayostahili NAMbie anatumia antibiotic gan
@ athma lakin
tatizo la moyo kama congenital heart ds. Kama tundu dogo kwenye moyo
lakin kama wk tatu ni pneumonia. But usiogope garama. Ni pm nikutumie namba yangu ya simu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom