Hivi inawezekana kwa daktari kuweza kung'amua kua unamatatizo au huna tatizo la moyo kwa kufanya vipimo vya damu tu na kusikiliza mapigo yako ya moyo?kama ni kweli ni vipimo gani hvyo vya damu ambayo atavipa priority kwenye kung'amaua tatizo?naomba kuwasilisha.
Kujibu swali lako ni HAPANA. si kwa vipimo vya damu na mapigo ya moyo vyenye kuweza kutoa majibu pekee.
Nikimaanisha "mapigo ya moyo" pamoja na vipimo vya damu viko sawa lakini bado mtu akawa na tatizo la moyo.
Uwekaji wa vipaumbele hasa ni vipimo gani vya moyo vifanyike hutegemea historia ya tatizo, vipimo vya awali(kusikiliza mapigo ya moyo ikiwa ni mojawapo), n.k
Hata hivyo vipimo vitakavyofuata hutegemea mahali ulipo mf. Blood culture, X-ray, ECG, ECHO n.k