Ndo jibu la swali lake..??Nadhan Ukitaka ukimbie usumbufu wa mwenye nyumba jitaidi kujenga yako mkuu
Hiyo inakuwa added kwenye hela ya mwenye nyumba au inapunguzwa?Withholding tax ni kodi unayotakiwa kulipa TRA 10% ya fedha unazomlipa mwenye nyumba.Ni wajibu wa mpangaji na si mpangishaji kulipa withholding tax.
Hiyo inakuwa added kwenye hela ya mwenye nyumba au inapunguzwa?
Kwa mfano,
Pango ni Tshs 100,000/=
10% ni Tshs 10,000/=
Sasa
1. Jumla ya malipo itakuwa ni 110,000/- kwamba 100,000/= ni ya mwenye nyumba na 10,000/- ni withholding tax..??
2. Jumla ya malipo itakuwa ni 100,000/- kwamba 90,000/= ni ya mwenye nyumba na 10,000/- ni withholding tax..??
Withholding tax ni kodi unayotakiwa kulipa TRA 10% ya fedha unazomlipa mwenye nyumba.Ni wajibu wa mpangaji na si mpangishaji kulipa withholding tax.
Asante mkuu, nilipeleka swala hili serikali za mitaa, inaonekana hawajui sheria, kwanza walinifokea kwamba najifanya najua wakati sijui kitu. Wanasema mwenye nyumba (aliitwa pia) analipa kodi ya jengo, nikasema wanachanganya mambo kama kweli analipa kodi alete namba yake y mlipa kodi (TIN). Nikaonekana mkorofi nikafukuzwa na mwenye nymba kanipa notisi ambayo eti nilipe hiyo miezi ya notice.
Hiyo Withholding tax kwenye kodi ya nyumba ni kwa makumpuni tu haihusu watu binafsi.
Mkuu, WHT kwa sasa kwenye nyumba zetu huku za uswahilini sheria haitubani ukiondoa wale wa apartment registered na nyumba zinazopangishwa kama maofisi, wao wanapaswa kulipa WHT tena 10% na wakionyesha mikataba yao ofisi ya TRA, ila naona kuna utaratibu unaandaliwa wa kuweza watu kuja kulipia:Waungwana wana JF, nawapa salaam,
Ama baada ya salaam, naombeni busara kutoka kwa wabobezi wa maswala ya kodi (kama nilivyoonyesha kwenye kichwa cha habari hapo juu).
Naishi kwenye nyumba ya kupanga na nimekaa kwenye nyumba hii tangu 2008. Mwenye nyumba amekuwa na tabia ya kupandisha kodi kila baada ya miaka miwili jambo ambalo limenifanya niwe kwenye wakati mgumu.
SWALI LANGU: Hivi hii sheria ya withholding tax inawahusu wapangishaji nyumba za biashara na SI nyumba za kuishi?
Naombeni msaada wa kitaalamu kwa mwenye uelewa zaidi
Nawasilisha ombi.