heshima kwanu wanabodi,
Naomba msaada wa ufafanuzi namna TRA wanavyokokotoa mahesabu ya kodi yao. mimi nilikuwa mwajirika katika sekta binafsi na mkataba wangu uliisha dec 2012 na makusanyo yangu kwa muda wa miaka miwili niliofaya kazi yalikuwa ni jumla ya ya Tsh 2,800,000/=, kwa wastani wa Tsh 166,700/= kwa mwezi. Cha kushangaza ni kwamba TRA walichukua tsh, 800,000/ ambayo ni zaidi ya asilimia 29% ya gratuity yangu.
kutokana na maelezo hayo hapo juu naomba kupata ufafanuzi wa namna TRA wanavyokokotoa mahesabu ya yao ya kodi kwa kipato hicho.