Msaada; LUKU error 77 display

Kremme

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
471
Reaction score
495
Wanajamvi,

Naombeni msaada,

Umeme umeisha kabisa kwenye luku yangu kila nikiingiza TOKEN inatokea error 77. Msaada please.Tokeni namba zote ni sahihi kabisa.
 
weka mita kwenye socket hata kama umeme hakuna halafu
andika 0 halafu weka mita namba halafu weka tena 0 halafu weka mita namba tena then bonya kama unavowekaga luku
 
kama hyo ndo mita namba yako andika 024213190598024213190598

jumla ztakuwa namba 24 then ENTER

wakat unafanya hayo hakikisha hcho kidude kiwe kwenye socket

italeta salio la luku 0.00

halafu jaza luku
 
Ni mteja mpya? Kama ndio nenda ofisi za TANESCO kwa ajili ya kukusajili kwenye manunuzi ya Luku!!
 
Wanajamvi naombeni msaada umeme umeisha kabisa kwenye luku yangu kila nikiingiza TOKEN inatokea error 77. Msaada please.Token namba zote ni sahihi kabisa
Mkuu kukiwa na tatizo la kukatika umeme line yenu huwa inatokea hii error hata kama unit zipo. Subiri umeme urudi line yenu kisha weka token ya huo umeme uliouziwa. Fuatilia jirani waliungwa line hiyo au piga simu TANESCO.
 
kama hyo ndo mita namba yako andika 024213190598024213190598

jumla ztakuwa namba 24 then ENTER

wakat unafanya hayo hakikisha hcho kidude kiwe kwenye socket

italeta salio la luku 0.00

halafu jaza luku
Mkuu, yangu inaonesha REJECT ninapoingiza tokeni. Kwann?
 
Nadhani kuna tatizo hata jiran yangu anaingiza luku inaandika USED
 
Kwa upande wangu unakuta unit zipo ila kila ikifika saa nne au saa tatu usiku unakatika unarudi saa mbili au saa tano asubuhi kila siku kama formula.
Hizi luku ni majanga kwakweli
 
Kwa upande wangu unakuta unit zipo ila kila ikifika saa nne au saa tatu usiku unakatika unarudi saa mbili au saa tano asubuhi kila siku kama formula.
Hizi luku ni majanga kwakweli
umeme ukiwa mdogo hzo luku znajikata! kwa mie napenda kwa kuwa znaokoa vitu visiungue! ila tanesco uwaambie ili waongeze transformer eneo lenu
 
Niliisolve kesho yake, tatizo lilikuw spring ya betri ilikatika, hivyo ki-remote hakikuwa na chaji.
 
Niliisolve kesho yake, tatizo lilikuw spring ya betri ilikatika, hivyo ki-remote hakikuwa na chaji.
Na hilo ndio tatizo kubwa la hizi REMOTE....kukatika Spring za BETRI na ukiwaendea TANESCO hawana msaada ( kiufundi) zaidi ya kukupa maujanja wakikwambia uweke karatasi ya Sigara (ile inayokaa ndani ya paketi) Alminium....
 
Kwa upande wangu unakuta unit zipo ila kila ikifika saa nne au saa tatu usiku unakatika unarudi saa mbili au saa tano asubuhi kila siku kama formula.
Hizi luku ni majanga kwakweli
Nafikiri ni tatizo la Low Voltage.
Baadhi ya mita za LUKU zina viwango vya voltage inayotakiwa kutozidi au kupungua.
Umeme ukizidi/ukipungua relay ya mita ina command circuit breaker ikate mkondo wa umeme.
Wakati wa matumizi makubwa ya umeme (peak hours), voltage huwa ndogo hivyo ni lazima ukutane na tatizo hilo.
 
Hakikisha betri zako zina nguvu

Leo tarehe 30 - 1 - 2020 tokea saa mbili nimehangaika sana kuingiza luku ila ilikuwa inagoma, nimeenda hata kwa jirani wawili kuingizia ila imegoma, baada ya hapo nikakata tamaa, Nimerudi kwangu saa tatu nikaona labda tatizo ni betri, basi nikazing'ata betri ili ziongezeke nguvu nikaziweka kwenye mita, nikaingiza namba kitu kikajibu "good" na umeme ukawaka.

Nunua betri mpya au ziminye hizo betri kwa kuzing;'ata na meno, hakikisha umezifunga kwenye kitambaa kama utazibana kwa kuzing'ata na meno maana zinaweza kupasuka unapozing'ata na zikipasuka zina sumu kali sana
 
kama hyo ndo mita namba yako andika 024213190598024213190598

jumla ztakuwa namba 24 then ENTER

wakat unafanya hayo hakikisha hcho kidude kiwe kwenye socket

italeta salio la luku 0.00

halafu jaza luku
P-Cut meter yangu inasoma na umeme hauingii ndani tatizo nini
 
P-Cut meter yangu inasoma na umeme hauingii ndani tatizo nini

Hii ulijibiwa kiongozi, na mimi imetokea hii P-Cut umeme hauingii, ilianza kuwa unapiga dim dim alafu unakatika baada ya muda unawaka ila sasa hivi ngoma imegoma, kesho ndo nakwenda TANESCO ila niliamua ku-search kwanza mtandaoni ndo nikakuta hii post.

Yoyote mwenye info ya P-cut anipe maujuzi kabla ya kwenda TANESCO. Nafufua uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…