Zaburi 23
JF-Expert Member
- Feb 22, 2017
- 570
- 658
Kama picha inavyoonekana hapo, nasumbuliwa na hayo mabaka kwenye kende hapo. Vinawasha hatari sio poa.
Msaada wenu dawa gani inafaa?
=====
Maoni yaliyotolewa na mdau
Msaada wenu dawa gani inafaa?
=====
Maoni yaliyotolewa na mdau
------Hiyo ni chronic fungal infection. Inasababishwa mara nyingi na unyevu wa mara kwa mara wa meneo hayo, na pia hali ya uchafu kama vile kutumia boxer moja kwa muda mrefu bila kubadilisha, hasa maeneo yenye joto kama Dar.
Matibabu:
1.Kitu kikubwa cha kwanza, kabla ya matibabu yoyote yale ni kuzingatia usafi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kutovaa boksa kwa zaidi ya siku moja hasa kwa maeneo yenye joto kama Dar, pamoja na kuhakikisha kuwa unapomaliza kuoga, umejifuta vyema maeneo hayo, na pia unapomaliza kujitawaza kwa maji baada ya haja kubwa, unajifuta majimaji na taulo au toilet paper na kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni makavu kabisa.
2.Pili, kama unatumia chupi, nashauri uachane na chupi uwe unatumia boksa ambazo ni pana, zinapitisha hewa na ni za COTTON kwa 100% (hizi ni expensive zaidi, but ndizo ambazo zinashauriwa kiafya kwa usalama wa nyeti zako).
3.Tatu, wakati unatumia dawa, hakikisha kwamba boksa zako zote umeziloweka kwenye maji ya moto kabisa kwa muda wa dakika 15-20 kisha uzifue kwa sabuni, na kuzianika kwenye JUA, halafu kabla ya kuzivaa tena uzipige pasi vizuri.
4.Usivae boksa mbichi au yenye unyevu, pia hakikisha boksa zako unazianika kwenye JUA (sio ndani chini ya kitanda); Na hakikisha UNAPIGA PASI boksa kabla hujaivaa.
5.Kama una mpenzi wako ambae mnakutana kimwili, hakikisha pia na yeye anatumia dawa KABLA hujakutana nae tena (dawa za fungus za sehemu za siri kwa wanawake ni tofauti); Otherwise, utajitibu wewe, halafu ukirudi tena kwa mpenzi/mke wako, anakuambukiza tena, fungus zinarudi tena UPYA! Haya maelezo niliyokupatia ni muhimu sana ukayafahamu na ukayafuata,kabla na wakati unakunywa dawa, la sivyo kila siku wewe utakua ni mtu wa kunywa dawa za fungus.
Pole sana
Zaburi 23
-----Brother hiyo ni 'Pumbu erosion' almaarufu kama PE
wala haiambukizwi kwa njia ya mapenzi,bali ni kwa maji, hata hayo unayotumia kufulia boxa. Cha kufanya fua hizo boxa na maji moto acha zikauke halafu piga pasi ya moto mkali.
Tafuta zile dawa za mapunye za kupaka halafu paka na shinda ndani siku hiyo bila chupi acha kende zipigwe na hewa siku moja tu zinapotea.
-----Nenda duka la dawa kanunue SEPTRIN za elfu moja ni vidonge kumi utapewa.
Kisha nenda dukani kanunue mafuta ya kupaka aina ya BABYCARE ya kwenye kikopo kidogo kuliko yote bila shaka kina ujazo wa 25g na kinauzwa shilingi mia tatu.
Baada ya kununua hivyo vitu nenda nyumbani chukua vidonge vyako vyote kumi vya SEPTRIN visage viwe unga kabisa. Kisha changanya na hayo mafuta ya BABYCARE hakikisha unachanganya vizuri kabisa mkorogo wako.
Baada ya hapo oga vizuri jikaushe vizuri hizo korodani zako jipake mara mbili kwa siku yaani ASUBUHI NA JIONI. Endelea kupaka kwa siku kumi na nne (wiki mbili).
Na kuhakikisha mabadiliko utaanza kuyaona baada ya siku mbili tu DAWA HII NI YA UHAKIKA.
NOTE: usije changanya hiyo dawa na losheni. NARUDIA TENA USIJE CHANGANYA HIYO DAWA NA LOSHENI.
#usisahau kuleta mrejesho hapa.
-----Hiyo ni fagus mkuu inatokana na unapooga hujifuti maji vizuri au unavaa nguo zikiwa mbichi ilishawahi kunipata huwa vinawasha sana hasa wakati joto limezidi. Kuna dawa niliitumia ni ya kupaka iko mtindo kama zile dawa za macho za kuminya Hata dispensary Zipo nimesahau jina kdgo ni muda niliwahi kuitumia, unapata mara tatu kwa siku baada ya wiki tuu fresh. Kaulizie bei nadhani ni elf6
Mwanangu nenda duka LA madawa.
Ukishafika duka la nadawa.
Mwambie muuzaji unataka Vidonge vya Griseofulvin dozi ya siku 28--30
Na Dawa ya kupaka inaitwa Clotrimazole cream.
Alafu mwangu ukishapata.
Kwa kutegemea athari ulizopata mwanangu kwenye pumbu (sijui km ngozi inakutoka (kutoka magamba) pumbu kuuma n.k..sijui ni kwa muda gan
Ila utachagua kati ya haya mwanangu
1---Unywe kimoja kila siku kwa siku 28--30
2---Unywe viwili Mara moja kila siku kwa siku 14--15
3--Unywe Kimoja Asubuhi , kimoja jion kwa siku 14--15 .
Wakati huo huo ukipaka iyo cream asubuh na jion .... Safisha eneo LA pumbu kwa maji vuguvugu au ya kawaida tu. ,hakikisha unapafuta panakauka kabisa ndio ulale Dawa.
Hakikisha unabadili Boksa kila utavyokua unapaka Dawa.( kama unaboksa 2--3) basi haki kisha unaifua nakuinyoosha kabla ya kuvua.
Kumbuka, usafi wako namavazi ndio kuta kufanya upone kabisa mwananguuu.
Kinyume nahapo hazitaisha ng'ooooo mwanangu.
Mwisho wasiku ,UTAOGOPA HATA KUGONGA MWANANGU..maana ukigonga tuu, Siku mbili tatu demu ataanza kulia 'Baby nawashwa hahahah, baby natoka na uchafu hahahahah