Msaada: Magonjwa hayaishi toka utotoni

Kacharimbe

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
216
Reaction score
35
Wakuu,

Nimeamua kuomba ushauri baada ya kusumbuliwa na magonjwa kwa muda wa zaidi miaka 30 sasa. Tangu nianze kujitambua, sijawahi kaa zaidi ya mwezi bila mwili wangu kuwa na maumivu sehemu

Nikiugua hiki kitaniandama wee, nikikitibu kinaanza kingine, naanza kutibu. Kikipona kinaanza kingine. Nitoe mifano michache. Nakumbuka nilisumbuliwa sana na kipanda uso.

Nikatumia dawa mbalimbali na kupona baada ya mwaka hivi. Baadaye ikaja miguu, ikanisumbua sana, nikapona. Likaja tumbo usiku tu, nikiamka mzima. Usiku ukiingia nashtuka saa 8 ni tumbo kuuma hadi asubuhi.

Orodha ni ndefu sana ikiwemo Malaria Typhod Amoiba na UTI.Mpaka leo hii nina 40 yrs mwendo ni ule ule nikipona Malaria Typhoid, nikipona Typhoid Malaria. O level na chuo kikuu nilikuwa natumia muda mwingi Dispensary.

Nafuu nilipata nikiwa Alevel. Afya yangu ni nzuri tu na sijawahi kudhoofika sasa mimi sina imani na mambo ya ushirikina lakini wakati mwingine nimekuwa nikitaka kuamini mambo hayo.

Kuna nini hadi siishi kuwa na maumivu/ugonjwa. Nadhani kwa wastani kati ya siku 7 za wiki, sita nakuwa na dozi dawa.

Nimeleta kwenu ili niweze kupata mawazo na uzoefu
 
I can feel ur pain. Pole sana. Jaribu kutumia vyakula vinavyoongeza immunity ya mwili. Again pole sana
 
Pole sana mkuu,fuata ushauri hapo juu ni mzuri,Mungu akutie nguvu.
 
Mhhhh, ngoja nipite tu...ila pole sana mkuu.
 
hauna sickle cell labda ukacheki maana watu hao wanasumbuliwaga na magonjwq
 
I can feel ur pain. Pole sana. Jaribu kutumia vyakula vinavyoongeza immunity ya mwili. Again pole sana

Asante mkuu. Mwaka 2012 nilijaribu hilo kwa takribani miezi 8 ikiwa ni pamoja na kuacha vyakula vya mafuta na nyama za kuchoma, but didnot make any difference
 
mkuu hebu tumia sana vyakula kama dawa sio tu eti kichwa kikiuma umeze paracetamol, pia fanya mazoezi asubuhi najioni, ota jua asubuhi na pia ukiweza uwe unaamka saa tisa au kumi usiku,toka nje au hata dirishani,juta hewa mara nyingi na kutoa kwa robo saa kila siku...utaona maajabu..
uzizoee madawa
 
Habari mkuu tibalishe za kuongeza kinga zipo, ni mitishamba lakini ipo in form of capsules. ni combinationa inapatikana kwa 90,000. Ukiitaji nicheki kwa 0719 252523
 
Ushari wangu mimi kama unavuta sigara achakuvuta Sigara kama unakunywa Pombe acha kunywa Pombe fanya mazoezi kwa wingi. Kunywa sana maji ya Uvuguvugu kila siku unapo amka asubuhi kunywa glasi3 kabla ya kula

kitu kisha kaa kwa muda wa saa 1 bila ya kula kitu baada ya saa kupita waweza kunywa chai. Na wakati wa mchana kunywa tena kama ulivyo kunywa asubuhi ila utakunywa Maji ya uvuguvugu glasi2 tu na ukae kama ulivyo kaa asubuhi.

Na wakati wa usiku kunywa tena kama ulivyo kunywa wakati wa mchana maji ya uvuguvugu glasi 2. Na wakati wa kulala utakunywa maji ya uvuguvu glasi 1 kisha ndio ulale fanya hivyo kila siku hutauguwa na maradhi. Dawa ingine kula kila siku

asubuhi punje 2 za kitunguu saumu na wakatiwa usiku kula tena punje 2 za kitunguu saumu hutoumwa na maradhi yoyote yale ukihitaji tiba zangu bonyeza hapa.Mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…