Msaada: Maisha ya Mgonjwa wa Figo anayefanya dialysis

Msaada: Maisha ya Mgonjwa wa Figo anayefanya dialysis

Wingawinga

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
623
Reaction score
1,531
Je, mgonjwa wa figo ambaye zimesha haribika na yuko kwenye dialysis huwa maisha yake yakoje? haswa mgonjwa aliye kijana na mwanaume. Je, huwa anaweza ishi maisha ya kawaida, yani kufanya mazoezi kwenda gym, kujenga misuli?

Je, kwenye msuala ya sex anakuwaje, anauwezo ule ule au unapungua?
 
Mkuu

Hata sisi wazee hatuombi Mungu tukutane nayo!
Najua mkuu,hakuna mtu anaeomba ugonjwa..namaanisha hayo magonjwa kukutana nayo ujanani unapoteza future mapema,unaweza Kuta mtu Hana mtoto then anakutana nayo... uzeeni fainal Kinga za mwili zishachoshwa ujanani na mapombe,mavyakula ya viwandan,hukwepi hayo
 
Je, mgonjwa wa figo ambaye zimesha haribika na yuko kwenye dialysis huwa maisha yake yakoje? haswa mgonjwa aliye kijana na mwanaume. Je, huwa anaweza ishi maisha ya kawaida, yani kufanya mazoezi kwenda gym, kujenga misuli?

Je, kwenye msuala ya sex anakuwaje, anauwezo ule ule au unapungu
Mkuu ninavyo juwa mimi Mgonjwa wa figo anayefanyiwa dialysis awe kijana au Mzee hana maisha marefu safari ya kifo inamsubiri muda sio mrefu. Kwani hiyo dialysis inasaidia kwa muda figo lako lipate kufanya kazi lakini haiwezi kabisa kutibu kufeli kwa mafigo yako Dawa ninayo ya kuweza kumtibu mgonjwa aliye feli mafigo yake na akapona kabisa ukihitaji nitafute kwa wakati wako ili niweze kumtibia mgonjwa wako na atapona kabisa kwa uwezo wake Mungu.
 
How long do dialysis patients live?
The average life expectancy on dialysis is 5-10 years. However, many patients have lived well on dialysis for 20 or even 30 years. Talk to your healthcare team about how to take care of yourself and stay healthy on dialysis.
Wagonjwa wa dialysis wanaishi muda gani?
Matarajio ya wastani ya maisha kwenye dialysis ni miaka 5-10. Walakini, wagonjwa wengi wameishi vizuri kwenye dialysis kwa miaka 20 au hata 30. Zungumza na timu yako ya huduma ya afya kuhusu jinsi ya kujitunza na kuwa na afya njema wakati wa dayalisisi.
 
Mkuu ninavyo juwa mimi Mgonjwa wa figo anayefanyiwa dialysis awe kijana au Mzee hana maisha marefu safari ya kifo inamsubiri muda sio mrefu. Kwani hiyo dialysis inasaidia kwa muda figo lako lipate kufanya kazi lakini haiwezi kabisa kutibu kufeli kwa mafigo yako Dawa ninayo ya kuweza kumtibu mgonjwa aliye feli mafigo yake na akapona kabisa ukihitaji nitafute kwa wakati wako ili niweze kumtibia mgonjwa wako na atapona kabisa kwa uwezo wake Mungu.
Asante sana , nit kutafuta kujua tuna msaidiaje ,sababu ndio kaingia kwnye vipimo , bado hatujajua kama ni anatakia kufanyiwa dyalisis ama la , ninashukuru sana .
 
Je kuna mtu yuko kwnye dialysis au ana mtu wa karibu yake anafanyiwa dyalisis atueleze vizuri experience ikoje? asanteni
 
Mkuu ninavyo juwa mimi Mgonjwa wa figo anayefanyiwa dialysis awe kijana au Mzee hana maisha marefu safari ya kifo inamsubiri muda sio mrefu. Kwani hiyo dialysis inasaidia kwa muda figo lako lipate kufanya kazi lakini haiwezi kabisa kutibu kufeli kwa mafigo yako Dawa ninayo ya kuweza kumtibu mgonjwa aliye feli mafigo yake na akapona kabisa ukihitaji nitafute kwa wakati wako ili niweze kumtibia mgonjwa wako na atapona kabisa kwa uwezo wake Mungu.

Usimtapeli mwenzio
 
Je kwenye masuala ya mapenzi dyalysisi ina athari nguvu za kiume?
Hii mbona priority ya kipumbavu sana. Hivi mtu anayepigania maisha yake nguvu za kiume zinakuwaje priority? Ushenzi mwingine ni wa kishenzi kweli. Hayo matibabu tu ni stress tosha za kumfanya mtu ngono isiwe kipaumbele.

Huna chakula siku ya nne sasa njaa inataka kukuua halafu unauliza kama unaweza kuvimbiwa au ukapata constipation. Ngono hufanywa kwa ufasaha pale afya ya mwili na akili inapokuwa sawa.
 
Kwa mtu ambaye ana ugonjwa wa figo ambazo zimesharibika na anahitaji kufanyiwa dialysis, maisha yanaweza kuwa na changamoto kadhaa. Dialysis ni mchakato wa kuondoa uchafu na sumu kutoka kwenye damu kwa kutumia mashine maalum ambayo hufanya kazi ya figo. Dialysis inakuwa sehemu muhimu ya maisha yake, na inahitaji kufanyika mara kwa mara, mara nyingi angalau mara tatu kwa wiki. Hii inaweza kusababisha mabadiliko katika mtindo wake wa maisha na kumzuia kufanya baadhi ya shughuli.

Kuhusu kufanya mazoezi na kwenda gym, uwezo wa mgonjwa utategemea hali yake ya kiafya. Inashauriwa kuwa na mazoezi ya wastani na kufuata ushauri wa daktari wako. Baadhi ya wagonjwa wa figo wanaweza kufanya mazoezi ya mwili kwa kiasi fulani, kulingana na hali yao na ushauri wa wataalamu wa afya. Hata hivyo, mazoezi yenye nguvu sana yanaweza kuwa ngumu zaidi kwa sababu ya uchovu na udhaifu unaoweza kusababishwa na ugonjwa wa figo na dialysis.

Kuhusu maswala ya ngono, uwezo wa kijinsia unaweza kuguswa na hali ya ugonjwa wa figo na matibabu ya dialysis. Kwa wanaume, uwezo wa kudumisha ujinsia unaweza kupungua kutokana na uharibifu wa figo na mabadiliko katika viwango vya homoni. Hata hivyo, hii ni ya kesi kwa kila mtu na inaweza kutofautiana kati ya wagonjwa. Ni muhimu kuzungumza na daktari wako kuhusu wasiwasi wowote au mabadiliko unayoyapata katika maisha yako ya ngono ili upate ushauri sahihi na ufahamu wa hali yako binafsi.

Ni muhimu kukumbuka kuwa kila mtu ni tofauti, na athari za ugonjwa wa figo na dialysis zinaweza kutofautiana kati ya watu binafsi. Ni vizuri kushauriana na timu yako ya matibabu ili kupata mwongozo sahihi kulingana na hali yako ya kiafya na mahitaji yako binafs
 
duh, mgojwa anaogopa dyalisi ana hizi naweza nguvu za kiume zikafa, hajafikia stage hiyo ila an ahofu sana, sijui kwa sasa kama an aimamisha maana kumuuliza na shinwa ila ana hofu akifikia stage huyo na ni kijana wa miaka 25
Dialysis hawezi kuiepuka, labda kama akibadilishiwa figo, Dialysis ni ya kusukuma siku tu ziende...
Itammaliza kila kitu...
 
Back
Top Bottom