Mkuu,
Pole sana kwa mgonjwa na familia kwa ujumla.
Mgonjwa anayefanya Dialysis anapaswa kubadili mwenendo mzima wa maisha. Kuanzia kwenye machaguo ya chakula na hata mfumo mzima wa maisha. Vyakula vyenye Calcium na potassium kwa wingi anapaswa kuviepuka. Vinywaji pia vinapaswa kuwa kwa uangalifu mkubwa.
Juu ya swala la mazoezi, hii inategemeaa na mazoezi yenyewe. Wagonjwa wa kufeli kwa figo hujihisi wachovu sana. Mazoezi mazito hayapaswi kuwa sehemu ya machaguo yao. Mazoezi mepesi labda anaweza kuyafanya. Ila yale ya vijana ya kunyanyua chuma vizito hapana.
Kuhusu swala la kushiriki tendo la ndoa, anapaswa kuelewa kwamba uwezo wake hupungua. Kushiriki tendo, mtu anapaswa kuwa sawa kisaikolojia, awe na nguvu za mwili na mwili uwe na maji ya kutosha. Wagonjwa wanaofanya dialysis, anakuwa kwanza na uchovu. Pili, wengi huathirika sana kisaikolojia. Na kiwango cha intake ya maji, hutegemeana na hali na hali.
Kwa minajili hiyo, uwezo wake wa kufanya mapenzi hupungua sana.
Anachopaswa kuelewa mgonjwa wako ni kuwa, kufikia dialysis, anachopaswa kukipa kipaumbele ni afya yake. Ni hatua ya kusogeza maisha mbele. Ngono si swala la muhimu sana. Kama ana mwenza, naye anapaswa kumuelewa mpenzi wake katika hali hiyo.
Kujumlisha na hilo ni kuwa, dialysis pia huambatana na matatizo mengine kadhaa. Si sahihi sana kumueleza mgonjwa, kwa sababu utamletea hofu zaidi.
Mungu awasimamie.