msaada: majina na vyuo katika nchi zilizoendelea vinavyokubalia mtu aliyefanya degree kwa miaka 3

msaada: majina na vyuo katika nchi zilizoendelea vinavyokubalia mtu aliyefanya degree kwa miaka 3

Skillseeker

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
225
Reaction score
34
Habari zenu wanaJF,
Ninatafuta vyuo katika nchi zilizoendelea kama UK,USA,Canada,New Zealand na zinginezo ili niweze kupata nafasi ya kusoma masters katika mambo yahusuyo IT. Nimejaribu kufanya utafiti lakini katika hatua yangu ya awali ya utafiti wangu katika tovuti mbalimbali nimeona kuwa vyuo vingi sheria yake ya kwanza ni kuwa ukitaka kuapply ni lazima uwe umemaliza degree iliyokuchukua miaka minne(4). Kwa watu waliosoma nchi kama Tanzania, India, Kenya, Uganda n.k. degree nyingi hutolewa kwa miaka mitatu tu..

Ninaamini kuwa uwezekano wa kusoma katika nchi zilizoendelea kwa mtu aliyemaliza degree yake kwa miaka mitatu upo sababu wanafunzi wengi kutoka nchi za africa wanakwenda huko kila mwaka.

Je, vyuo gani ambavyo vinakubali hata mtu aliyesoma degree ya miaka mitatu?
Jinsi gai mtu aliyesoma degree ya miaka mitatu anaweza akaingia hata katika vyuo vinavyohitaji mtu aliyemaliza degree ya miaka minne?..
naomba mnisaidie kwa hili..

natanguliza shukrani...
 
Back
Top Bottom