Msaada: makato CRDB

Msaada: makato CRDB

Alpha Blondy

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
304
Reaction score
440
Wakuu nahitaji msaada wa maelezo kwa yeyote anaejua haya makoto.

Ipo hivi nilifungua account ya CRDB bank ile ya furahaa account kwa maelezo yao, kuwa haina makato ya kila mwezi,
Nikakaa muda kidogo kama miezi mitano bila kuitumia, nikawa nimesahau password,

Leo nikaenda bank ku reset password, wakaanitaka nilipe Tsh 2999, nikalipa nakufuata process zote, wakaniambia nikabadilishe kwenye mashine ya ATM,

Kabla ya kwenda kwenye Kubadilisha kwenye ATM nikadeposit 1,000,000 nikiwa ndani ya benk, nikatoka na kwenda kubadili Password kwenye mashine ya ATM nikabadili nilipo angalia salio nikakuta limebaki 996,300 yan imepungua 3,700.
Kwa yeyote anayejua kwanini nimekatwa hicho kiasi aniambie
 
Kwa case yako hii kwa nini usingewauliza hapohapo benki??..au ulienda ATM tofauti na hiyo ya hapo branch??
 
Ilikua ni jioni sana mimi nilikua mteja wa mwisho kutoka nisingeweza kurudi ndani, ila kesho nikiwa na nafasi nitaenda kuuliza
Naenda kauluze uko tuache sss tuko busy na maswala ya kina kinana
 
Ilikua promotion ah ah Equity bank wenyewe had I account za biashara Hanna makato...jifunze kufanya utafiti kabla kufanya maamuzi
 
Labda gharama ya card ya ATM..
Ila mkuu huko vizuri.
Wengine sisi milango ya benk ni kama milango ya mahabusu
 
Labda gharama ya card ya ATM..
Ila mkuu huko vizuri.
Wengine sisi milango ya benk ni kama milango ya mahabusu
Kwa kiasi flani mzee ila nimeikusanya kwa kuweka akiba kwa muda mrefu tangu mwezi wa kwanza si unajua maisha ni kuunga unga, nina malengo flan ikifika kiasi flani nifungue kiofisi changu
 
Mabank yote yatakuambia hawana makato...hizo ni lugha za biashara (kuwahadaa wateja ili wakupate) bank zinapata faida kwa mikopo na makato...makato yapo ya aina mbali mbali mfano kutoa na kuweka fedha kuna makato, kutoa hela Atm kuna makato, kuna makato hupita kila mwezi mara moja ya kumaintain account yako, kuna makato ya kadi yako, n.k . Muhimu ni vizuri uulizie bank makato yote yaliyohalalishwa ni haki yako kuyafahamu.
 
Benki zote ziko kibiashara,na zipo pale ili watumie ela zako ili wao waendelee kustawi.....kama fedha zako kukaa benki hazikupi faida ni bora uzitowe ukazitunze/kuzitumia unapopajua
 
Back
Top Bottom