Msaada: Makisio ya gharama za ufundi wa kujenga nyumba

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
WanaJF naombeni Msaada,nimeshajenga Msingi nataka kupandisha nyumba yangu hadi juu kozi kumi kufunga Mkanda na kuweka kozi 3 juu ya Mkanda(Lenta) wa kusukiwa nondo 4,makisio ya matofali ni 3700,natarajia kumtumia Fundi wa kawaida Technician ila sina ujuzi wa gharama za Ufundi naogopa kuingiliwa,nilikuwa naomba mnipe mwanga kwa gharama za kawaida za kibongobongo lakini zenye ubora na tija natakiwa kumlipa huyu Fundi kwa kazi hiyo Tsh ngapi?Naombeni mnisaidie kunipa Mwanga wakuu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

mpatie milioni tatu
 
Mkuu,
Huwezi kujua gharama za ujenzi wa nyumba yoyote kama hujajua ukubwa wa nyumba yako.

Kwa hiyo kama una ramani ya nyumba yako leta hapa jukwaani au kama unaweza kumleta mtaalam wa uthamini akapima ukumbwa wa nyumba yako, ndio unaweza kupata uhalisia wa gharama ya ujenzi wa nyumba yako.

Vinginevyo utadanganywa tu!
 

nadhani makisio ya tofari 3700 yanaleta mwanga ukizingatia ameshamaliza msingi na anataka ifike mpaka kwenye mkanda tu na anataka gharama za fundi pekee....

Cha maana inabidi ajue gharama za fundi inategemea mahali fundi mwenyewe as well as ku bargain

ingawa wengine huwa wanacharge percent fulani ya gharama ya mradi kama ni kazi za kiserikali
 
mkuu kwakukusaidia tu nikwamba fundi wa kawaida anajenga tofarmoja kwa sh 300 lakin kufanyahivo anatakiwakua chin ya msimamizi kwaiyo ukimchukua fund unatakiwa kulipia sh 500 kama huyofundi hanakaz nyingi kwawakat huo naongea hivo kwasababu mimi ni fundimwashi mwenye uzoef na kaz hiyo kwa miaka10 naish dar .
 
Master Legendary:

Angalia jedwali hili linaweza kukusaidia.

Nimelitolea maelezo marefu hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-vyumba-vitatu-na-sebule-3.html#post11163200

Huko nimeweka mfano kamili ukiwa na ramani na jedwali la makadirio ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko na mabafu matatu. Unachotakiwa ni kubadili takwimu chache tu** kwenye jedwali la MS Excel kwa kulingana na ramani ya nyumba yako.

**(urefu wa kuta zote, upana na urefu wa madirisha na milango yote, eneo la nyumba yote)

NB:
  • Huu ni ujenzi wa mafundi wa mitaani.
  • Sijaweka gharama za kujenga msingi kwani unategemea mambo mengi sana.
  • Huwezi kupata mkopo kwa njia hii.

Hapa na pale nitaendelea kuiboresha hii programu/jedwali hili, lakini mpaka sasa nina imani litakusaidia kukupa mwanga kwenye gharama nyingi za ujenzi.

Cliff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…