Msaada: Makosa kwenye kujaza fomu ya pasipoti ya kusafiria

Msaada: Makosa kwenye kujaza fomu ya pasipoti ya kusafiria

navigator msomi

Senior Member
Joined
May 8, 2018
Posts
188
Reaction score
224
Wakuu samahani, naomba mwenye maarifa kidogo juu ya swala hili anipe mawazo kidogo.

Nilijaza fomu ya kuomba passport mtandaoni hadi mwisho kisha nikailipia then after nika download tayari kwa kui-submit ofisi za uhamiaji.

Tatizo langu ni kuwa baada ya kuidownload form nimeona picha niliyotumia haijakaa vizuri, yaani nilkosea wakati nina upload picha haikukaa poa.

Swali langu ni kwamba, je, naweza fanya chochote ku-edit picha au nitume maombi mapya?
 
Mfumo haukuruhusu kufanya marekebisho, itume kama ilivyo marekebisho watafanya wao.

Picha iliyoko kwenye fomu siyo itakayotumika kwenye Pasi ya kusafiria, watapiga nyingine hapo hapo itakayojumiisha mboni za macho yako na alama za vidole.

Kila lakheri!.
 
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom