Kwanza kabisa unapojaribu kutumia any beta version software ujue kupambana na mapungufu yake. Beta software ni kwa ajili ya majaribio tu na hutumiwa zaidi na wenye ujuzi wa taaluma hiyo. Kuhusu windows 8 kama kweli umeweza kuinstall kwenye computer yako basi utakua una utaalamu wa kujua hayo mapungufu, moja wapo ni kukosekana kwa drivers za computer yako; hata hao developer wa hiyo windows 8 yenyewe huwa hawana hizo drivers kwani wao pia huzipata from third party. Mara nyingi au at this stage of development ya software hushauriwi kutumia kwa production /daily use purpose. Hivyo kama ni computer ambayo unatumia kwa shughuli za kila siku basi rudisha O/S iliokuepo mwanzo au weka dual boot.