Msaada maswali juu ya utafiti wa ufugaji wa kuku wa mayai

Msaada maswali juu ya utafiti wa ufugaji wa kuku wa mayai

kajansi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
485
Reaction score
222
Wana jamvi heshima kwenu! baada ya kupata maelezo mengi hapa jamvini sasa nimeamua rasmi naanza kufuga kuku wa mayai. Kama kawaida kabla sijaanza ningependa kuwatembelea wafugaji,wataalam, na wadau wengine nikitaka kujua mengi kuhusu ufugaji huo. Ninataka kuandaa kitu kama questionnaire ili kupata majibu ya watu hao nitakaowatembelea, msaada ninaoomba kwenu ni je niwaulize vitu gani ili viweze kunisaidia kuanza kwa ufanisi kazi hii?

KARIBUNI SANA WAUNGWANA!
 
Je unataka kufuga wa biashara au kwa ajili ya lishe ya familia tu lazima uwe specific!
Utafugia eneo gani la hapa Tz ukiwa umelenga soko gani?
Ukubwa wa mtaji wako ni kiasi gani ili kujua kina cha kukushauri!
Kama ungekuja na draft yako kwanza ungepata msaada mkubwa watu wangejazia mapungufu vinginevyo yaani unahitaji uandikiwe maelezo mengi sana. Hata hivyo wazo lako ni zuri sana naamini michango itapatikana tu JF!

Niwie radhi kwa maelezo marefu mimi nami sinaga dogo mweeee!!
 
Back
Top Bottom