msaada matatizo ya ngozi kwa mtoto

Jmturu

Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
56
Reaction score
9
habari wanajamvi,kwanza kabisa poleni na majukumu ya kila siku pili hongera kwa kuzaliwa tanzania na kuongeza idadi ya waafrika. nikirudi ktk topic nduguzanguni nahitaj msaada wa ushauri ni nini cha kufanya kwa huyu mtoto anaeteseka tangu kuzaliwa kwa mwaka na miezi 7 sasa. ana tatizo la kutokwa na vipele vigum km vya joto lkn havijali hali ya hewa. vina tabia ya kukauka na kutoka vingine bila kumuacha apumzike hata kidogo. nimejaribu kumbadilishia mafuta ya kupaka mara kadhaa km vile samona,jonhson baby,vaseline na ht babycare lkn tatizo limesimama pale pale. nimelileta kwenu wana jf huenda nikapata utatuzi km inavyokua kwa mengine.
 
1.Tafuta dawa inayoitwa hydrocortison na Locoid ointment umpake mara mbili kwa siku(asubuhi na jioni)with a thin layer kwa siku saba.Hio hydrocortison utumie usoni kama ana vipele hapo,Epuka kumpaka karibu na macho na hio locoid ointment mpake mwilini..
2.Ukimuogesha mtoto tia neutral oil kwenye beseni la maji,hii itasaidia ngazi isikauke,ikiwezekana muache maji yakauke yenyewe (air dry)usimfute na taulo
3.Epuka kutumia sabuni zenye harufu,iwe ya kuongea au ya kufulia na Mafuta/cream zenye manukato vilevile
4.Mvalishe mtoto nguo za cotton tu.
 

Luv u kwa hayo majibu yako, duh unaonekana ni mlezi mzuri kama sio daktari!
 
Aisee nakushukuru sn mimi49 kwa msaada wako. Tatizo limepungua kbs naamini tunakoelekea litakwisha kbs.mungu akubaliki sn.
 
Pole, nashauri watafute watu wanaofanya kazi na kampuni ya forever living, hata mie unaweza kunitafuta, mi nafanya kazi sector ya afya na nina uzoef na siyo mgen na hayo mambo, ipo siku utajua kwa nini nimekudirect forever living products kwa kurahisha mawasiliano tumia 0752720276
 
Asante kwa majibu mazuri, kwa ushauri mzuri
Naomba kuongeza machache

Maelezo uliyompa ni sahihi kabisa, na more likely ni atopic eczema/allergy, inaweza kusababishwa na vyakula (so aangalie mtoto anamlisha nini-the common allergen kwa watoto ni nyama, samaki, maziwa ya ng'ombe, mafuta, sabuni, mafuta ya kupaka na hata nguo ambazo sio pure cotton)

Hivyo ajaribu kuchunguza ni kipi kati ya hivyo kinamwathiri mtoto, kwa msaada zaidi anaweza kwenda hospitali akafanye allergy test.

Ila uzuri ni kwamba hizi allergy za watoto zinapungua au kwisha kadiri umri unvyozidi, baada ya miaka 5, matatizo haya ni mara chache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…