MahakamaniNimehitimu diploma katika chuo cha kati cha private fani ya mifugo mwaka 2022.
Baada ya matokeo kutoka mimi pamoja na wenzangu (classmates) tukiangalia verification zetu NACTE tunaonekana tumeishia kusoma mwaka wa 1 semister 1.
Tukiulizia chuo tunaambiwa wao chuo matokeo tayari walishapeleka Nacte ila tukienda nacte wao wanatujibu hawajapokea matokeo toka chuoni kwetu kwa muda mrefu.
Tunawaza kuchukua hatua za kisheria ila hatujui ni wapi hasa tunaanzia, tunaomba ushauri wenu mwenye uelewa na hili ni wapi tunaweza kupatiwa usaidizi wa kisheria ili tupate haki yetu.
Ahsante!
Ahsante kwa ushauriKwa uzoefu wangu, shida iko chuoni na wala Sio nacte, mambo ya kukosa matokeo au namba ya mtihani ni ishu za chuo, kuna mawili ni uzembe wa chuo au ujuaji wa wanafunzi (UKIJIFANYA MJUAJI SANA CHUONI WALIMU WANAKUKOMOA TU ) ,namna ya kulitatua mkamshike mkono mwalimu mmoja kwa siri atawasaidia ikishindikana kabisa nendeni mahakamani.