Msaada: Maumivu upande wa bega la kushoto, juu kidogo ya moyo

Msaada: Maumivu upande wa bega la kushoto, juu kidogo ya moyo

Ina Hu

Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
47
Reaction score
18
FF. Doctors heshima kwenu,

Mimi ninasumbuliwa na matatizo ya maumivu upande wa bega la kushoto, juu kidogo ya moyo.

Nimekuwa nikisumbuliwa na hii shida kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu na hapa nishaenda muhimbili kupata vipimo ikaonekana upande wa moyo hakuna shida, vipimo ya damu yaani full blood picture ilionesha colestro na pia uric acid ilo juu kwahiyo ninashida ya gout.

Nikapewa dawa lakini bado hali si nzuri miezi inaisha. Pia nimecheki vidonda vya tumbo nimeambiwa ni reactive, so nikapewa herigo kit for two weeks ninamalizia leo. Shida ni hayo maumivu na sometimes kichwa kinauma kwa mbali.

Thanks in advance
 
Pole Sana ndugu,
Tatizo kama lako lilinitokeaga miaka ya nyuma, sababu hasa ilikua ni msongo wa mawazo uliopitiliza. Njia pekee iloniponyesha ni kuondosha hizo stress. Hali ilipotea yenyewe bila ya kutumia dawa yoyote ile. Japokua ninapopatwa tena na mawazo mengi hali hiyo hunirudia japo kwa mbali.
Nikushauri tu kama inatokana na stress jaribu kuzipunguza ndugu.
Ahsante.
 
hili jibu huwa ninalipata ninajaribu kuwa normal lakini ninajikuta hii hali haijatulia, sijajua hasa nifanye nini kupoteza hayo mawazo
 
Mimi ndio imenianza km week mbili nyuma kama muda wa siku tatu nikaambiwa ni presha imeshuka labda nikaenda kupima iko normal nikaambiwa ninywe maji kwa wingi ile hali ikapotea
 
Japo hilo suala la msongo wa mawazo nahisi pia linamchango mkubwa sana ktk tatizo hilo
 
Hilo ni tatizo la watu wengi sana sasa hivi cholesterol inasumbua sana watu wengi na inaumiza sana mwili viungo vyote vitauma na uchovu mwingi hali kadhalika vidonda vya tumbo vinadalili hizo hizo hasa acid kama ipo juu hivyo fuata masharti ya lishe kuzuia acid isiendelee kumwaga nyingi na tumia dawa za vidonda vya tumbo lakini kubwa ni masharti ya kula usitumie vyakula vyenye acid kama nyanya ndizi za kupika viazi mviringo vyakula vyote vyenye mafuta mengi maziwa majani ya chai kahawa nk
 
Back
Top Bottom