Msaada, mawazo na uzoefu biashara ya asali

notyfeky

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
713
Reaction score
730
Wazoefu tufahamishane yafuatayo kuhusu biashara ya asali mbichi:
  • Ipi njia ya kuifahamu asali nzuri?
  • Upatikanaji wa asali, wapi inapatikana nzuri na kwa wingi? Bei ya kununua kwa mzalishaji sh. ngapi?
  • Je kuisafirisha kutoka mikoani kwenda kuiuza Dar kuna ulazima niwe na kibali?
  • Bei ya kuuza Ikoje? Lita sh.ngapi kuuza?
  • Changamoto za biashara hii ni zipi?
  • Kwa Dar es Salaam soko lake liko wapi?
N.b;
Nataka kuanza kuifanya hii biashara, naomba wazoefu waje kutoa muongozo.
Karibuni.
 
Unaitambua kwa vipimo vya mositure content pia jinsi inavyomiminika na kutumia njia zingine kama njiti ya kibiriti au utambi. Asali inapatikana zaidi huko Chunya na Tabora kwenye misitu ya miombo, bei ya jumla ni kati ya shs 5,000 hadi 10,000 kwa lita bei ya kuuza ni shs 15,000 kwa lita. Vibali ni muhimu na kuna taratibu zake, bishara ina soko kubwa na inalipa sana ukizingatia. Dar kila sehemu unaiuza inategemea unauza kwq style gan na umelenga wateja wa aina gani.
Karibu sana katika biashara hii
 
Ahsante mkuu.
Utaratibu wa vibali ukoje? Kibali kinakatiwa wapi na gharama zikoje?
Nataka kuanza na Lita20 kusafirisha Dar, je kwenye gari wataniulizia kibali?
 
Ahsante mkuu.
Utaratibu wa vibali ukoje? Kibali kinakatiwa wapi na gharama zikoje?
Nataka kuanza na Lita20 kusafirisha Dar, je kwenye gari wataniulizia kibali?
Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu au vizuia vya Maliasili. Dumu la lita 20 ni shs 3,000 hivi kibali chake.
 
Mkuu nakucheki Pm, kwa ufafanuzi zaidi
 
Nakata kuwa wholesaler wa asali wapi nitapata soko la uhakika (ma retailer) au consumer wa mwisho tufanye biashara…asali yangu natolea tabora
 
Nakata kuwa wholesaler wa asali wapi nitapata soko la uhakika (ma retailer) au consumer wa mwisho tufanye biashara…asali yangu natolea tabora
Mkuu nenda Morogoro mjini pale soko la Kingalu, mimi ndo nilikuwa naacha mzigo wangu pale baada ya wiki naenda kusanya kibunda cha kutosha. Pia unaweza watumia wanafunzi wa vyuo vikuu kama vile UDOM, SUA, MU, UDSM na wengine huko kuna soko sana pia.
Hii biashara soko lake ni pana mno, inategemeana nawewe tu jinsi umeiplan.
 
Mkuu hakuna mtu unaefahamiana nae apo soko la kingalu unipe ata mawasiliano yake ili nifanye nae biashara.

Hyo ya mavyuoni nitajaribu mkuu
 
Mkuu hakuna mtu unaefahamiana nae apo soko la kingalu unipe ata mawasiliano yake ili nifanye nae biashara.

Hyo ya mavyuoni nitajaribu mkuu
Mda mrefu sana, jamaa nikuwa nafahamiana nae sina mawasiliano yake pia nipo mbali na Moro. Ukifika pale we onana na wenye maduka.
 
wapi huko wanauza asali 15000 kwa lita
 
Biashara ya asali huuzwa kwa kipimo cha kilo si lita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…