dogojanja 87
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 882
- 213
Katika harakati za kupambana na ugumu wa maisha nimenunua shamba maeneo ya rufiji ambako mhogo unalimwa,nimeishasafisha shamba nataka kulima mhogo kwenye msimu huu wa mwezi wa 11 (vuli).changamoto ninayoipata ni mbegu.shamba langu ni eka 10,mpaka sasa nimepata mbegu za kutoshea eka 3,mwenye kujua zinapopatikana mbegu hizi kwa urahisi anisaidie maana msimu ndi huooo unaanza.