Msaada:Mbegu za mhogo

dogojanja 87

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
882
Reaction score
213
Katika harakati za kupambana na ugumu wa maisha nimenunua shamba maeneo ya rufiji ambako mhogo unalimwa,nimeishasafisha shamba nataka kulima mhogo kwenye msimu huu wa mwezi wa 11 (vuli).changamoto ninayoipata ni mbegu.shamba langu ni eka 10,mpaka sasa nimepata mbegu za kutoshea eka 3,mwenye kujua zinapopatikana mbegu hizi kwa urahisi anisaidie maana msimu ndi huooo unaanza.
 
Nenda kwenye kituo cha kilimo cha karibu nawe

Kuna mbegu mpya wamezigundua siku hizi zinazohimili magonjwa na kutoa mazao mengi.
 
Mikocheni na Kibaha. Pia na Mkuranga. Wadau wengine ambao.utapata Mbegu ya kutosha ni Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele- Mtwara. Huko utapata mbegu za kutosha.

shukrani sana kaka,kwa mikocheni panaitwaje na ni sehemu gani specifically?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…