Msaada Mbegu za Papai Malkia F1 zimegoma kuota

Msaada Mbegu za Papai Malkia F1 zimegoma kuota

Negemu

Senior Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
136
Reaction score
138
Niko kwenye majaribio ya kilimo cha papai,aina ya malkia F1, nilinunua packet moja ya mbegu, ambayo ina mbegu 80, hatua ya kwanza niliziloweka kwenye chombo chenye maji safi kwa muda wa suku 5 na kila suku nilikuwa nabadilisha maji, siku ya 6 nikahamishia hizo mbegu kwenye kitambaa cheupe kisafi kilicholoana nikazifunga kwa pamoja,na kuziweka juu ya sahani kwenye meza kwa siku 5, huku nikiloanisha kwa maji kidogo kila suku kwa muda wa siku 5,siku ya sita nikafungua kikakuta baadhi ya mbegu zimepasuka, nikahamishia kwenye viriba nilivyokuwa nimejaza udongo uliochanganyika na mbolea iliyooza,nilichimba shimo dogo kwa kutoboa na kijiti na kuweka mbegu mojamoja kwenye kila kiriba, nimekuwa nikimwagilia kila siku tangu tarehe 31/5/2019 mpaka leo tarehe 24 sijaona dalili yeyote ya kuota, sijui nilikosea wapi
IMG_20190624_100432.jpeg
IMG_20190523_183157.jpeg
 
Ushawahi kuotesha hz mbegu kwa mtindo huu hapo kabla? Nahisi umezidisha siku za mbegu kukaa kwny maji / kitambaa. Halaf kingine packaging date ya hiyo mbegu kidogo inanipa mashaka ina miaka miwili tangu itengenezwe kuna uwezekano germination percentage imepungua.
Cha kufanya beba hiyo pact yako pamoja na risiti rudi kwa muuzaji aliekuuzia na umpe feedback!
 
Hizo papai nimelima Sana tatizo lake hazidumu zinazaa Sana mwanzoni Kisha Basi

Alafu Ni ngumu Sana kuota ila nilikuwa napambana nazo Hadi zinaota , sometimes nilikuwa naziania juani na hata hicho kitalu kinataka jua pia

Siku nyingine otesha tu hizi za kienyeji mkuu
 
Nami nimelima papai cha kufanya nunua papai moja kubwa kata kati ndani ya papai zina mbegu aina mbili nyeusi tii na za kijivu hizi nyeusi ni dume zitenge mbali na hizi za kijivu na weka hizi za kijivu kwenye bakuli kubwa tia maji mpaka juu utaona mbegu zile zinazoelea juu juu ni zile dhaifu zikipandwa zikiota zinakuwa dhaifu ila zile zilizozama chini ndiyo imara zaidi hizi ndizo unaotesha kwenye viliba na baada ya wiki moja zimeota.
 
Mkuu unaotesha bila kukausha? Zitaota?
 
Back
Top Bottom