Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kama huna utaalam wowote wa kum-handle mbwa anayetaabika, iwe ni kwa sumu au ajali yoyote bora ukubaliane na matokeo.Jirani yangu Mbwa wake Vibaka wamemuwekea sumu,Amekufa anamuangalia hajui afanyeje! Nahofia na mimi hawa wa kwangu,Maana wananisaidia sana na Hawa panya road wa kitaa.
Ahsante, Ingawa umenisimanga!Mkuu kama huna utaalam wowote wa kum-handle mbwa anayetaabika, iwe ni kwa sumu au ajali yoyote bora ukubaliane na matokeo.
Lakini Kama una ABC's za wanyama hatari (mbwa akiwa ni mmojawapo) waweza kutumia mkaa uliosagwa kwa kumnywesha kama hatua ya Awali. Waweza pia kutumia maziwa fresh na Kama unauzoefu na sio mwoga, tumia Atropine sulphate injectable na mpumzishe na usimsumbue wala kujaribu kumtapisha.
NB: Kuwa mwangalifu sana kwani anaweza kukujeruhi vibaya.
Dah! Mkuu; Pole sana haikuwa nia yangu kabisa kukusimanga. Kwa bahati mbaya katika Taaluma hatukuzoeshwa kulainisha lugha. Naomba uniwie radhi mkuu kama nimekukwaza. Ilikuwa ni kwa nia njema tu aisee. 🙏 🙏Ahsante,Ingawa umenisimanga!