Msaada: Mdogo wangu yupo darasa la 6 ila jina limetoka kwenye matokeo ya darasa la 7 ikidaiwa jina lake liliuzwa

Lakin majina mengi si yanafanana jamani
 
Ushauri wangu .naomba ufuatilie sasa usipofuatilia alafu ukakuta hilo jina ni la mdogo wako. Tatizo kubwa Moja litatokea mwakani wakati anasajiliwa ili afanye mtihani was taifa drs la 7 ni kwamba itahitajika matokeo yake ya mtihan wa taifa drs la 4 na necta kule itaonekana jina Hilo limeshamaliza drs la 7 hivyo dogo hataruhusiwa kufanya mtihani. Siku hizi hakuna udanganyifu necta wapo kidigital mzee hakuna uhuni uhuni.
 
Watu wengine bana. Majina hufanana. Mi primary nilikuta nafanana jina na mtu mi nikabadili
 
Acha papara mdogo wako yuko darasa la sita na aendelee na darasa la sita,aliyekwambia jina ni mali ya mdogo wako ni nani? Majina hufanana,mdogo wako atafanya mtihani mwakani period.
 
Mtoto akirudia darasa taarifa zinaenda mamlaka husika na anapata kibali.Kama utaratibu ulifuatwa hakuweza kuwa na tatizo.Ushauru,mleta mada kamuone mwalimu mkuu wa shule anayosoma sasa mdogo wako ndo atakupa majibu mujarabu,ikishindikana nenda halimashauri kwa Afisa Elimu.
 
Mzee baba jina ambalo halina hata cheti cha la7 liuzwe kwa faida gani!? Acha mawazo potofu....


Majina hata manne yanaweza fanana! Matatu kitu gani?
 
ww umejuaje kama walicheza mchezo mkuu.
Usijazwa upepo mkuu mambo mengine sio ya kukurupuka, kumbuka jina halina dhamana yeyote anaweza kujiita kadili anavyopendezwa.
.


hapana mdogo wangu hakuwa mtoro kabisa isipokuwa walimu walicheza mchezo haram
 
Je, jina la mdogo wako kutoka limefaulu mwaka huu, linamzuia yeye kuchaguliwa kuendelea na masomo mwakani kama atafaulu? Aliyefaulu kwa jina hilo achana naye, wala usiwe na kinyongo naye
 
Hii ngumu sana ila kwa sasa huwezi kuuza jina
 
Majina yanafanana, umejuaje ni la mdogo wako.
Unaweza fananisha majina matatu maana mtu anatambulika kwa jina lake la baba na la ukoo kwahyo yote yafanane au umetoka kuchambia pilipili umekuja kutafuta unga wa ngano tukakusugue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…