Msaada:Meno yangu hayajaota katika mpangilio unaotakiwa

Msaada:Meno yangu hayajaota katika mpangilio unaotakiwa

Salamu kwenu wanafamilia ya JamiiForums...

Natumaini mna uzima tele....kama hivyo ndivyo basi tabasamu kama ishara ya upendo na furaha yako.

Dhumuni la kuandika uzi huu ni hitaji nililonalo juu ya tatizo linalonikabili.

TATIZO LENYEWE:
Meno yangu hayajaota katika mpangilio unaotakiwa (nje ya nafasi)
inapelekea baadhi ya matatizo kwangu

a:Nashindwa kutafuna vizuri
b;Usafishwaji mgumu wa meno
c;tabasamu lisilo na mvuto
d;matatizo ya kisaikolojia
e;Nashindwa kuzungumza vizuri

HITAJI;
JE! Ni wapi naweza kupata matibabu ya gharama nafuu(natoka katika familia duni)

njia gani nitumie ili kufanikisha matibabu

Pia CHOCHOTE UNACHOWEZA KUNISAIDIA ili kupata matibabu

Akhsanteni!

Sidhani kama unapashwa ulalamike au ujisikie vibaya kwa huo mpangilio wako mbaya wa Meno / Njino bali unatakiwa umshukuru pia Mungu kwakuwa hayo meno yako na hivyo unavyosema yalivyo Siku ikitokea tatizo lolote lile labda umekabwa au umedhulumiwa basi ' ukimng'ata ' nayo Mtu ndiyo ' ntolee ' hiyo breki Kaburini tu Kuzikwa. Huna tena haja sijui ya kumiliki ' bastola ' au kutembea na ' kisu ' badala yake meno yako hayo ni ' Silaha ' ya maangamizi tosha.
 
Naonaga wahindi huwa wanafunga nyanya kwenye meno huenda ikawa ndio solution ya kuyaweka meno katika mpangilio mzuri,bei zake sizijui kabisa.
 
Siku ukikutana na kibogoyo asiye na meno ndio utajua thamani ya hayo meno yako hata kama hayana mpangilio unaotakiwa.
 
Unasema unashindwa kutafuna vizuri,kwani chakula hua unatafunia meno ya mbele?!
 
Hayo meno yanakunyima tabasabu dear? Nimechek avatar nkagundua unajitakia matatizoo, iko romantic hivyo na hiko kirangi chake. Relax, jifunze namna yakuswaki vizuri uwe na amani
 
itanigharimu kama kiasi gani cha fedha ili nijipange

shukran!
Ni ghali sana mkuu, imagine kupata jino moja tu la bandia lenye root and crown (bandia lakini likiwekwa halitoki na linakua kama jino OG) sio chini ya USD 2000.

Hivyo kama unahitaji huduma za cosmetic surgery ni gharama sana we jitahidi kuendana na hali yako tu. Hapo kama ni tokea utoto basi kulikuwa na uzembe kwa upande wa wazazi maana ungewahiwa kulikuwa na uwezekano ungekuwa na dental formula nzuri tu.
 
Meno yako yanatibika vizuri sana mkuu!! Unatakiwa kuwa na shilingi laki sita kuyanyoosha yote.

Meno ya juu ni laki tatu, na ya chini laki tatu. Lakini pia unaweza ukaamua kuyanyoosha meno ya juu peke yake ambapo ni shilingi laki tatu tu. Unawekewa mawaya fulani majino yote yanakaa mkao sawa sawa.

Ukitaka kuyapiga rangi yawe meupe pia nadhani ni shilingi laki mbili kwa meno yote pale muhimbili.

Nakutakia matibabu mema.
 
Inategemea na mahali ulipo mkuu. Karibu kila mkoa una hospital atleast yenye kitengo cha kusafisha meno. Dar es salaam kuna hospital nyingi sana za kuweka sawa meno.

Usikubali kujinyima tabasamu mkuu.. tafuta dentist akunyooshe hayo majino mkuu
 
Meno yako yanatibika vizuri sana mkuu!! Unatakiwa kuwa na shilingi laki sita kuyanyoosha yote.

Meno ya juu ni laki tatu, na ya chini laki tatu. Lakini pia unaweza ukaamua kuyanyoosha meno ya juu peke yake ambapo ni shilingi laki tatu tu. Unawekewa mawaya fulani majino yote yanakaa mkao sawa sawa.

Ukitaka kuyapiga rangi yawe meupe pia nadhani ni shilingi laki mbili kwa meno yote pale muhimbili.

Nakutakia matibabu mema.
shukrani sana mkuu!
 
Back
Top Bottom