kidodosi hiyo ardhi uliinunua kwa nani?
Kuna taratibu za kununua ardhi kijijini. Wewe na aliyekuuzia mnaenda serikali ya kijiji, wanajadili maombi yako ya kutaka kununua ardhi, wakiridhika wanapeleka maamizi yao kwenye mkutano mkuu wa kijiji ili mamuzi yapitishwe au vinginevyo.
Vikao vyote viwili, yaani s/kijiji na mkutano mkuu wanaandika mihutasari ya maamuzi na nakala unabaki nayo.
Na unapotaka kununua ardhi ya kijiji ambacho wewe si mkazi unahitaji udhamini wa wanakijiji saba, wake kwa waume.
Mlifanya hivyo? Tuanzie hapo..
nipo barabarani nimeshindwa kuquote vifungu ila waweza kujisomea sheria ya ardhi ya kijiji namba 5 ya 1999 na kanuni zake ukipata.