Msaada miguu inavimba

Msaada miguu inavimba

tembocard

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
247
Reaction score
121
Habari zenu?

Naombeni ushauri nilikuwa naumwa na typhoid na vidonda vya tumbo kwa muda wa kama wiki 2 hivi na sasa hivi bado nipo kwenye dozi ila cha kushangaza toka Jana naona miguu inavimba na ninapata maumivu sasa nashindwa kuelewa tatizo ni nini au ni sindano niliyochomwa kipindi naumwa nilichomwa vibaya maana toka nichomwe sindano bado naskia maumivu kwenye tako.

Naombeni mawazo yenu ili nijue pakuanzia
 
Kaa kwenye kochi uweke miguu kwenye stool . Kama ni tatizo la circulation litakwisha
 
Asante mpenz, nikae kwa mda gani
anza sasa hivi mpaka saa ya kulala ukiamka unakwenda chooni tu. lakini pia muone daktari.

Miguu kuvimba ni dalili kuwa moyo haifanyi kazi kama inavyopaswa.
 
anza sasa hivi mpaka saa ya kulala ukiamka unakwenda chooni tu. lakini pia muone daktari.

Miguu kuvimba ni dalili kuwa moyo haifanyi kazi kama inavyopaswa.
Asante ngoja nianze sahivi kukaa
 
Back
Top Bottom