Hahaha... mkuu..
Sisi tulikaa giza more than a month hadi tukazoea kabisa.
This is what happens, watakuja watasema hyo mita n mbovu .
Then atakuja mwingine ambae atadema a different problem.
Atakuja wa tatu ambae attakuja kukagua kama panfaa kuwekwa mita n.k.
Yaan n mizunguko kibao ndugu yangu.
Cha kukishauri, we piga simu ili waje kila siku. Ukiamka asubuh piga sim una tatizo, watakuja watarudi. Wakichoka unafungiwa mita. Leo asubuh nenda ofisini waambie unafanya biashara ya samaki na wanaoza kwenye fridge kwaio wanakutia hasara.
Asipokuelewa mwambie nataka kuongea na meneja (ni haki yako).
Mkubwa akisema, wanakuja wanakimbia
Mkubwa akisema, wanakuja wanakimbia
Duh pole hiyo kitu ilinitokea kama miezi miwili hivi mita Yao iligoma tu kwa makusudi kuingiza token. Nilikuwa napiga simu sijui inapokelewa Dodoma kwanza halafu wao ndio wanawaambia watu wa huku nipo aisee nadhani nilipiga simu zaidi ya mara 50 ndani ya wiki mbili nilizokaa giza. Kwanza walikuja emergency wakasema ishu mita hivyo wanapeleka taarifa kitengo cha mita hapo ndio mziki sasa wale jamaa wanakupigia simu kabisa tunakuja halafu hawaji ukipiga simu unaambiwa tupe namba ya taarifa baadae unaambiwa taarifa yako haionekani ngoja tufungue taarifa upya hapo umeshakaa wiki mara utatumiwa ujumbe tatizo lako limeshughulikiwa huku hata fundi hajafika mwisho wa siku niliamua kwenda ofisi Yao kuu ya kanda nikamuona boss wao nikamwambia waje wang'oe mita Yao kabisa nitafanya application upya na nilikuwa na hasira maana wale jamaa wa emergency walipokuja walinisimanga sana mara njia yenu mabovu mnatia hasara kwa serikali kuja huku mara unanunua umeme mdogo unatakiwa kuweka umeme wa kuanzia 50K .baada ya kumuona boss wao hapo hapo alipiga simu kwenye ofisi yao inayohudumia sehemu nilipoona ndani ya saa moja mafundi mita walinipigia simu wapo jirani na kwangu nikawaelekeza yaani ni kitu cha dakika 10 wameshabadirisha mita umeme unawaka na wakasema mita ilikuwa imechoka