MSAADA: Mjamzito kusumbuliwa na gesi na tumbo kukaza sana.

kibuyu180

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2016
Posts
1,717
Reaction score
1,823
Wapendwa wana JF wenzangu habari zenu? ningependa kwenda moja kwa moja kwenye hitaji naomba mnisaidie mawazo nini nifanye kuhusiana na hali anayopitia Mke wangu ana mimba ya miezi minne anasumbumiwa sana na gesi, kiasi cha tumbo kumkaza sana kila anachokula kinamletea gesi.

Pia anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo yaani akibahatika ni kidogo mnoo ndo sababu pia ya tumbo kumkaza(kumuuma).

NB: Nilimpeleka hospital akaandikiwa dawa ya Kupunguza gesi Relcer Gel hata alipoanza Clinic aliandikiwa hiyo hiyo dawa. Inamsaidia kwa muda mfupi mnoo.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu. Naamini nitapata msaada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na shida za mke wetu.
Vipi ana history ya hilo tatizo au ni sub effects za ujauzito???
 
Hili tatizo huwa linawakuta sana wa mama wajawazito na huwa ni kawaida sana kwao kutokea.

Hata mke wangu iliwahi kumtokea alifika miezi minne ya ujauzito wake , Nilienda hospital doctor akashauri ajitahidi sana kula vyakula laini na matunda kwa wingi ili kusaidia hilo tatizo lipate unafuu.

Ilisaidia kidogo ingawa haikumaliza tatizo na alipojifungua alirudi kwenye hali ya kawaida tu.
 
Pole, mpe mapapai kwa wingi na maparachichi.

pia hiyo hali ni kawaida.
Hapa ndo tunavutana. Papai namwambia ni tunda zuri sana kwa Mazingira yake, mwenzangu anagoma. Kagoogle kasikia papai halifai kwa mama mjamzito. Linaleta abortion.
Binafsi sijakubaliana nae siwezi kumforce ale asichopenda ama kuridhika nacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Kaka kwa maelezo yako mazuri. Ntafanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ht mm niliacha tu, ila itafika time hali itakuwa shwari tu. Mwenyewe nilihangaika sana na hata mood ya kula ilikuja baada ya kuwa mimba iko na miezi mitano kuelekea sita ndio hali ikatulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana dada angu kwa maneno yako ya faraja nimepata faraja kujua kumbe wapo mliopitia hii hali ni mimba yake ya kwanza, hatuna uzoefu sote. asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana dada angu kwa maneno yako ya faraja. Nimepata faraja kujua kumbe wapo mliopitia hii Hali. N mimba yake ya kwanza, hatuna uzoefu sote. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Usijali ndg yangu, mwambie tu awe mvumilivu. Mimba zinasumbua sana hasa kipindi cha mwanzo, ajikaze tu kwsbb itafika time atasahau kbs hizo shida. Kadri mimba inavyokua na karaha ndogo ndogo zinapungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi hiyo hali inanitokea ni mjamzito wa miezi 4 napata changamoto mno na choo na pia uwa navimbiwa Mara kwa Mara ila dokta kaniambia kawaida tuu, sema nilipata shida nyingine ya kubleed week iliyopita hospital nimeenda mtoto yupo vzr na kila kitu naambiwa hii hali itaisha yani naogopa Mwenyezi Mungu anitetee tu nataman mno kuwa mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itaisha, ni suala la muda tu. Ht mm nilihangaika sana ila kwa sasa hali imekuwa fresh.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…