Msaada: Mke wangu anaelekea kunifilisi

Msaada: Mke wangu anaelekea kunifilisi

SHAMAC

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
1,343
Reaction score
3,561
" Yasini! Ingawa wazazi wangu wamekataa mimi kuolewa na wewe lakini moyo wangu umekuridhia wewe, nitaishi na wewe kwa shida na raha " yalikua ni maneno ya Saida kwa mpenzi wake Yasini miaka 10 iliyopita.

Yasini ni kijana mwenye ulemavu wa macho yote ( kipofu ). Yasini amekua kwenye maisha ya taabu mno lakini hilo halikumzuia Saida kumpenda, na kumkataa kijana aliyechaguliwa na wazazi wake awe mumewe.

Siku zikapita miaka ikasogea ndani ya ndoa ya kipofu na mwanamama mwenye haiba ya sura na umbo, ambaye hakuna kijana angezuia tamaa yake kuwaka pindi tu amtiapo machoni mwanamke huyu. Watoto wakajaaliwa Mwenyezi Mungu si mchoyo wa fadhila.

Baada ya mihangaiko mingi ya utafutaji Mungu si athumani, wananyanyuka from 0 to hero. Kipofu anakua zimba (pedezhee). Dunia na vilivyomo vinamwandama Yasini, mabinti wanajisogeza, pombe inamkolea. Anaanza kuisahau familia yake taratibu, migogoro ndani haikati mguu, ni daily.

Wafanyakazi wa kike kazini kwake ama kwa hakika hakuna ambaye hakuonja utamu wa Yasini. Yasini huyu huyu aliyekuwa kapuku, kipofu na kuonwa kwa macho ya roho na binti aliye na macho yote ya mwili, anageuka mbwa mwitu mwenye njaa kali na mambo dunia, hasikii wala haambiliki.

Mke anachoka anachukua maamuzi ya ghadhabu ya kumkomoa kipofu. Anajivutia njemba ya ukweli yenye macho yote na mwili wa kazi. Kijana anakabidhiwa jukumu la kumkuna mwanamama barabara, naye anajiachia kwa hasira zote.

Kipofu anagundua anaamua kufunga mdomo. Mwanamama anavuka mipaka anaileta njemba ndani, kipofu anaingia na la hasha kipofu si kiziwi anasikia miguno juu ya kitanda chake mwenyewe, sauti ya mkewe akigugumia kwa mautamu inapasua ngoma za masikio yake, anaamua kujifanya kiziwi angali ni kipofu toka tumboni mwa mamaye.

Mapenzi ya bi dada yanapamba moto anamjengea Bungalow mchepuko huyu anayeindesha akili yake, anamwanzishia biashara mchepuko na ama kweli kijana analia kivulini.

Waswahili wanasema walimwengu hadaa dunia shujaa. Hapo ndipo Yasini aliishia na kuweka kituo akinitaka nimsaidie kuwaza afanye nini kunusuru mali zake.?

Nilibaki mdomo wazi nisijue nini cha kumshauri kaka yangu mwenye ushawishi wa ajabu aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, licha ya kukosa cha kumshauri nilijifunza mengi sana juu ya zawadi za Mungu kwa mwanadamu.
 
Kwani alipokuwa anaponda maraha na vimwana yeye hakufilisi? Yeye alivyokuwa akila bata aache na mwenzie ale hawezi kumaliza zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom