Msaada mke wangu anataka kuniua

Msaada mke wangu anataka kuniua

litutumbwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
642
Reaction score
1,303
Nimechoka saaana, mke wangu, mama watoto wamgu, kipenzi changu, anataka kuniua

Leo asubuhi amenipikia mtori na maziwa, nyama kilo moja, akanitengea yote kwenye poti moja kubwa, nikala kwa mbinde nikamaliza

Mchana huu amepika nyama nusu kilo amenikaangiana viazi ulaya, nimekula kwa mbinde nikamaliza

Nimekaa for two hrs analeta jagila juice, kwa mbinde nikamaliza
yN

Nyama zote zilikua nammafuta mengi mno, na anajua hali yangu, mimi ni mnene mno.

Hapa nimelala chali naemea juujuu tu...jioni amepanga anipe chips yai na kidari

Jamani ananiua huyuuu
 
Na atakuua kweli.

Huo ubonge na bado anakujaza hiyo mivyakula nawe unaifakamia, matokeo yake ni kitambi+pressure+moyo+sukari nk, matokeo yake huwezi kupeleka moto, anaishia kuchepuka, unagundua/unamfuma pressure inapanda, moyo unashtuka, sukari inapanda, unapata stroke na kukata moto ghafla
 
GXwA3CZWEAAZEUL.jpg
 
Wewe litutumbwe nyuzi zako zote ni za masihara.

Huna tofauti na ile stori ya yule jamaa mchungaji ng'ombe msituni ambaye kila siku alikuwa anawasumbua wanakijiji kwa kupiga ukunga "Chui! Chui! Chui!"

Wanakijiji wakija kumuokoa, Anabaki kuwacheka kumbe hamna hata chui.

Siku chui alipokuja kweli, na kuanza kupiga ukunga Chui! Chui! Chui! Aliachwa peke yake akafa.

Hakuna mwanakijiji aliyejisumbua kwenda kutoa msaada.
 
Back
Top Bottom