Msaada: Mke wangu hashiki ujauzito

kitaalam baada ya miezi sita unaanza kuwa na ? hivyo ni vema kupima; na kikwetu kwetu walau mwaka mkuu, haraka ya nini ada unayo mkononi?

Miezi 6 mbona mapema?

Next time nunueni ovulation kit mpime kuona anaingia lini.

Lakini je mlishaenda na mwenza wako kupima? Wote wawili mnatakiwa mchekiwe
 
Hivi nyinyi wavulana wa mikoani mbona mnatuhaibisha hivi, wanaume tumeumbwa na makoromeo kazi yake ni kuficha siri, sasa jambo dogo tu la ndani ya ndoa tayari liko mtaa wa saba. Embu tupe number yake alafu uone kama hatapata mimba
 
Vp ushapima DNA maana kwa mujibu unaweza ukaambiwa ni yako ili usikate tamaa ya maisha
 
Miezi6 tu?! Mapema mnoooo
 
Jaribu na wewe kufanya sperm analysis, usimlaumu mkeo, lakini pia mpeleke naye kwa gynacologist ingawa miez sita si mingi ya kukupa presha.
Dah! Umenikumbusha kisa kimoja cha wanandoa.

Waliishi pamoja mwaka mmoja na nusu bila mke kushika mimba. Mume akavimba kwa hasira na kushusha kipigo kwa mkewe kwanini hashiki mimba.

Kuona vile bidada alitoroka na kutokomea kusikojulikana.

Baada ya mwaka kasoro hivi alirudi kwa wazazi wake akiwa mjamzito. Mungu akamjalia akapata mtoto. Akaenda tena huko alikokuwa akiishi. Sasa ana mtoto wa pili.

Kituko kwa yule kijana, alishaoa na kuacha wanawake wawili zaidi bila hata mimba. Mtaani kote hajawahi kusikika amempa bidada mimba.

Kabaki na aibu yake. Kumbe yeye ndiye tasa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…