Habari zenu wanajamvi. Jamani mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24 na nimebahatika kuajiliwa serikalini mshahara wangu sio chini ya laki 5 na wala haizidi laki 7. Mzee wangu alipata kununua eneo la ekari 20 huko mkoani Lindi katika wilaya moja ya Ruangwa. Shida yangu ni kama ninaweza kupata mkopo wa kilimo nikaliendeleza lile shamba au kama kunauwezekano nikakopa mkopo kupitia hilo eneo ili niweze kufanya shughuli nyingine za kibiashara basi mnisaidie namna ya kufanya niweze kutoka kimaisha uku kazini mkopo wa ki bank mpaka utimize miaka mitatu. Au kama kuna njia yoyote mbadala mnisaidie ili niweze kufika mbali asanteni.