Msaada:Mtoto anatapika maziwa aliyonyonya na mengine yanatokea puani!

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Salaam madokta wa humu

Mke wangu kajifungua mtoto wa kiume na kesho mtoto anatimiza miezi 3 kamili

Tatizo lililopo ambalo hata wife linamtisha ni Hali ya mtoto kutapikaga maziwa aliyonyonya na yanatokea puani

Yani mengine yanatoka mdomoni mengine yanatokea puani

Hali hi humtokea karibia kila siku ,Sasa nauliza nini chanzo cha hali hii na tiba yake ni ipi??
 
Miezi mi3 yote hujampeleka hospital? Au hilo tatizo lina muda gani
 
Lina muda kidogo,hospital aliambiwa tatizo litaisha lenyewe
 
Yah kutapika kwa watoto mara nyingi ni infection insitwa gastroenteritis lakini huwa inakwisha ndani ya masaa 48.
Angalia asiishiwe na maji mwilini, mpelekeni hospitali kubwa zaidi.
 
Huyo Mtoto Hacheulishwi!
Umeulizwa swali muhimu hapa, ule mtindo wa kumlaza mtoto kifudifudi baada ya kunyonya na kumpiga piga mgongoni ili acheue huwa mnafanyaga hivyo?
 
Umeulizwa swali muhimu hapa, ule mtindo wa kumlaza mtoto kifudifudi baada ya kunyonya na kumpiga piga mgongoni ili acheue huwa mnafanyaga hivyo?
Anacheulishwa,mamake nimemuuliza vizuri eti kaambiwa ni chango ,ila nataka niende mwenyewe hospital nikajue sababu sahihii ya Hali hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…