Homa si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa.
Homa inaweza kusababishwa na mambo mengi sana. Mathlani, kidonda tu kinaweza kusababisha homa kali.
Dhana ya kuwa homa inaletwa na malaria tu, siyo sahihi.
Mtoto mdogo hawezi kujieleza, yawezekana na matatizo katika sikio 'otitis media' au mkojo 'UTI' n.k
Ni vema umrudishe hospitali akafanyiwe uchunguzi wa kina kubaini sababu zinazopelekea joto la mwili kuongezeka.
Kuweweseka si dalili nzuri kwasababu homa inapozidi inaweza kusababisha hali hiyo. Na hali inaweza kwenda mbele zaidi na kusababisha dege dege 'convulsion'. Matokeo ya dege dege nayo pia si mazuri kwa afya na maisha ya siku za baadaye