hi doctors,kuna mwanangu ana umri wa mwaka mmoja sasa na sielewi kwann hapati usingizi.
yaani iwe mchana iwe usiku kulala ni kwa mbinde..mchana anaweza lala mara mbili lakini kila akilala ni kwa dakika zisizozidi 10-250 anaamka.
usiku akilala ni ananyonya usiku kucha na mama yake akiamka kwenda toilet na yeye anaamka,yaani mtu ukistuka na yeye anaamka.pia asubuhi na yeye anaamka kama anaenda kazini vile.hapati ule usingizi unaoitwa "wa mtoto mchanga"
naombeni msaada wenu huyu mwanangu anasumbuliwa na nini ktk umri huu mpaka usingizi wake uwe wa manati kiasi hiki:help::disapointed:
thank you in advance.